Kiongozi wa maandamano ya Ngorongoro ni nani? Polisi na Intelijensia hawakuona viashiria?

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
Kiongozi wa haya maandamano ni nani?

Polisi na Intelijensia walishindwa vipi kuyazuia kabla hayajaanza?

Kama wameshindwa kugundua maandamano makubwa kama haya, tuna uhakika gani na taarifa za kiintelijensia wanazodai kuwa wanazo?

..halafu Wamaasai walipiga mkwara Polisi wote wakanywea.

..Makonda, na kimbelembele chake, alijificha kwa siku tatu, na alipotokea alikuwa mpole.
Wewe usije kuwajaza wakadhani ni kweli wakija kuvuka red line usije ukaja humu kuanza kulilia haki za binadamu. Serikali haishindwi kitu ila siasa ina nafasi yake.
 
Jeshi la polisi limedhoofishwa kiuweledi na chama tawala,wamelitumia Sana kupambana na wasio na hatia kisa ni wapinzani!!!

Matokeo yake limeshindwa kujikita katika maswala mtambuka ya kitaifa!

Ishu ya wamasai nadhani ni mpango mkakati wa Dola kurejesha Imani ya wananchi kwao coz serikali imepoteza Imani Kwa wananchi ,wamebaki chawa walioishiwa nguvu ya uchawa wao!
 
..Kiongozi wa haya maandamano ni nani?

..Polisi na Intelijensia walishindwa vipi kuyazuia kabla hayajaanza?

..Kama wameshindwa kugundua maandamano makubwa kama haya, tuna uhakika gani na taarifa za kiintelijensia wanazodai kuwa wanazo?

Hawana lolote wanaloliweza labda kuhakikisha wanawadhibiti chadema wasifanye shughuki zao kikatiba.
 
Polisi wa kawaida wa kabila jingine asingeweza ku infiltrate jamii ya kimasai na kuchukua habari lakini pia hata polisi toka jamii ya kimasai asingeweza kufanya huo ujinga, maana wamasai wakiwa jandoni wanapewa kula kiapo Cha kutomsaliti mmasai mwenzake hata apewe kitu gani. Na angetokea msaliti wa kimasai Basi karma ingeanza na yeye.
 
Hii ndio point ya msingi..
 
..Kiongozi wa haya maandamano ni nani?

..Polisi na Intelijensia walishindwa vipi kuyazuia kabla hayajaanza?

..Kama wameshindwa kugundua maandamano makubwa kama haya, tuna uhakika gani na taarifa za kiintelijensia wanazodai kuwa wanazo?

Ungekuwa askari ungeua watu wengi sana, unaonesha haupendi watu wadai haki zao wanapoona wanaonewa.
 
Wewe usije kuwajaza wakadhani ni kweli wakija kuvuka red line usije ukaja humu kuanza kulilia haki za binadamu. Serikali haishindwi kitu ila siasa ina nafasi yake.
Usitishe watu bhana. Serikali imewekwa na wananchi. Wananchi ndio waajiri wa viongozi wote wa serikali. Wananchi Wana haki ya kupigania haki zao pale wanapoona zinapindishwa.
 
Polisi wa kawaida wa kabila jingine asingeweza ku infiltrate jamii ya kimasai na kuchukua habari lakini pia hata polisi toka jamii ya kimasai asingeweza kufanya huo ujinga, maana wamasai wakiwa jandoni wanapewa kula kiapo Cha kutomsaliti mmasai mwenzake hata apewe kitu gani. Na angetokea msaliti wa kimasai Basi karma ingeanza na yeye.
Ila wamaasai kama Fred Lowassa sio wa kuamini maana hao hawakwenda jandoni bali walifyekewa Agha Khan hospital na ndio maana pamoja na ubinge wao kwa jamii ya wamaasai hawatii Neno kutetea
 
Usitishe watu bhana. Serikali imewekwa na wananchi. Wananchi ndio waajiri wa viongozi wote wa serikali. Wananchi Wana haki ya kupigania haki zao pale wanapoona zinapindishwa.
Wewe endelea na ngonjera hizo wewe ndio umeajiri basi ungejiajiri mwenyewe. Nenda barabarani na kumbuka kuwaambia mimi ndio nimewajiri watakuomba uwaongezee mshahara.
 
Kiongozi wa haya maandamano ni nani?

Polisi na Intelijensia walishindwa vipi kuyazuia kabla hayajaanza?

Kama wameshindwa kugundua maandamano makubwa kama haya, tuna uhakika gani na taarifa za kiintelijensia wanazodai kuwa wanazo?

Kwahiyo unaona ni sawa watu kukatiwa huduma zote za kijamii , jifanye ungekuwa huko . Usingeandika hiki ulichoweka hapa
 
Kiongozi wa haya maandamano ni nani?

Polisi na Intelijensia walishindwa vipi kuyazuia kabla hayajaanza?

Kama wameshindwa kugundua maandamano makubwa kama haya, tuna uhakika gani na taarifa za kiintelijensia wanazodai kuwa wanazo?

Kiongozi wa haya maandamano ni nani?

Polisi na Intelijensia walishindwa vipi kuyazuia kabla hayajaanza?

Kama wameshindwa kugundua maandamano makubwa kama haya, tuna uhakika gani na taarifa za kiintelijensia wanazodai kuwa wanazo?

Kukiwa na sababu inayowaunganisha wote, mgomo na maandamano hulipuka bila kiongozi.
Ni KWELI kabisa, shida ndiyo imewaunganisha Wamasai.
 
Back
Top Bottom