Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,903
- 1,360
Kwa kuwa katiba ya nchi hii inatambua kuwepo kwa mihimili mitatu ya dola, yaani serikali, Bunge , na Mahakama, na kwa kuwa mihimili hii mitatu inapaswa kufanya kazi bila kuingiliana ila kuchungana, na kwa kuwa kiongozi wa mhimili wa serikali ni Rais, na kiongozi wa mhimili wa Bunge ni Spika, ambao wote ni viongozi wa CCM ngazi ya juu (ina maana tayari mihimili hii miwili imeshaingiliana), naleta hoja kuwa ili mhimili wa tatu (mahakama) usivutwe kuingiliana na hii miwili basi kiongozi wake ajiunge na Chama cha upinzani na epewe nafasi ya kuwa kiongozi katika ngazi za juu.
This will ensure checks and balances of the system.
Vinginevyo, kwa kuwa kiongozi wa mhimili wa serikali lazima awe kwenye chama cha siasa huyo aendelee kuwa kiongozi katika chama, ila kwa kuwa kiongozi wa mhimili wa Bunge si lazima awe mwanachama wa chama chochote cha siasa, sawa na ilivyo kwa kiongozi wa mhimili wa Mahakama, naleta hoja kuwa mtu yeyote akisha chaguliwa kuwa spika basi ajivue uanachama wa chama cha siasa na nyadhifa zote za kisiasa ili aweze kuongoza vizuri bunge ambalo ni la wananchi wote; vivyo hivyo kiongozi wa mhimili wa mahakama asiwe mwanachama wa chama chochotecha siasa.
Nawasilisha

Last edited: