Kiongozi wa nchi msafi hawezi kamwe kuongoza nchi iliojaa viongozi wezi. Rejelea Sani Abacha wa Nigeria

Kiongozi wa nchi msafi hawezi kamwe kuongoza nchi iliojaa viongozi wezi. Rejelea Sani Abacha wa Nigeria

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Kiongozi Msafi katika Taifa loloe lile kamwe na Daima haijawahi tokea akaongoza Taifa liliojaaa wapigaji wa mali za Umma.

Kule Nigeria inaaminika Gen Sani Abacha kwenye utawala wake kulikuwa na upigani ambao haujawahi fikiwa hadi leo, Kila kiongozi alikuwa anakula kwa urefu wa Kamba yake. Mtendaji wa kijiji Nigeria alikula kwa levo za Kijiji, Mtedandaji wa Kata akala kwa levo za kata, Wakuu wa wilaya wakala kwa levo za wilaya, wale wa Mkoa wakala kwa levo za mkoa na wale wa Taifa kwa levo za Taifa.

1720709695076.png
Abacha utawala wake ulijaa utoroshaji mkubwa sana wa pesa za Nigeria, yeye mwenyewe na wasaidizi wake kama Mawaziri na pia utakatishaji mkubwa sana

Abacha mwenyewe na Familia yake inaaminika walipiga $5 bilion, ingawa kiwango kinadaiwa ni zaidi ya hapo. Ila ukiweka na za washikaji zake wote kiwango ni kikubwa sana.

Hadi sasa pesa zilizo rudishwa ni zaidi ya $ Billion 6 ikiwa ni pamoja na Mali na cash.

Abacha aliongoza genge la upigaji kuanzia yeye mwenyewe hadi Mwenyekiti wa kijiji. Utawala wake ulijaa kuoneana sana aibu,kulindana kwa kwa sababu za kiasiasa na yeyote alie kosoa ufisadi alishughurikiwa.

Sasa basi hakuna sehemu yoyote ile Kiomgozi wa nchi akawa msafi akaongoza nchi yenye wapigaji, kuna uhusiano mkunwa sana kati ya Ufisadi wa nchi na viongozi wanao tawala.

Ukiona Viongozi au watendaji wanapiga pesa za umma katika Taifa lolote lile na wananyanaziwa, wanaonewa aibu wana lindwa jua kabisa kuna namna sio bure.

"Ukiona watoto wa simba wanacheza cheza wenyewe pembeni ya kichaka jua kabisa Mama yao yuko ndani ya kichaka katulia. Haiwezekani wacheze nje bila mama yao kuwa jirani nao kwa ajili ya kuwahami na adui yoyote yule"
 
Nchi za kiafrica system zote zimekuwa corrupted, kila anaepata nafasi basi anaitumia ipasavyo.
 
Tanzania haiwezi kuwa na kiongozi mkuu msafi, kwa sababu ngazi ya kupandia kufika juu kwenye uongozi imejaa uchafu.
 
Wizi ni wizi tu, utawala unaoingia madarakani kwa wizi wa kura hauwezi kukemea aina yoyote ile ya wizi. Ni hayo tu.
 
Back
Top Bottom