Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga amerejea Nairobi baada ya kumalizika kwa ziara ya kibinafsi huko Dubai.
Raila ambaye amepokelewa na aliyekuwa kinara mwenza wake katika Uchaguzi Mkuu uliopita Martha Karua, anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la Kibra kabla ya kuhutubia Wanahabari katika mgahawa wa Serena.
Raila anarudi Nairobi huku kukitarajiwa vuguvugu jipya la maandamano dhidi ya serikali kuanzia wiki ijayo.
Kwengineko Rais William Ruto amemuonya Odinga kuwa atamchukulia hatua za kisheria iwapo atarudi barabarani kufanya maandamano.
Odinga vilevile anatarajiwa kugusia tukio la Jana ambapo polisi walirusha vitoa machozi karibu na Ofisi za Chama cha Rais mstaafu Uhuru Kenyatta katika eneo la Kileleshwa. Tukio hilo lilipelekea Kenyatta kwenda mpaka Kileleshwa kutoa 'amri' ya kuondoka kwa maafisa wa polisi, jambo ambalo alifanikiwa kufanya.