East African Eagle
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 3,759
- 2,206
Kama ilivyo kawaida Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) likianzisha operation yake nje ya nchi lazima lishinde.Likiwa kongo liliweza kuwakimbiza mbio kongo na kuwavurumisha waasi wa M23 ambao wana asili ya Rwanda na kuwatokomoza wasiendelee kuonea wananchi wa kongo.
Safari hii JWTZ inapambana na waasi wa Uganda wa kundi la ADF-NALU kule kongo.ADF-NALU wakajitia wanatikisa kibiriti kwa JWTZ kwa kuushambulia msafara wa JWTZ na kuua askari wawili wa Tanzania.Kilichofuata hapo ni mshike mshike.JWTZ kwa kushirikiana na raia wema,polisi na vyombo vya usalama wamemdaka kiongozi wa kundi hilo Jamil Mukulu na amefikishwa mahakamani Kisutu dar es salaam tarehe 16/05/2015 akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamevaa nguo za kiraia.Mwasi huyo aliyebadili dini kutoka ukatoliki na kuwa mwislamu jina lake ambalo amekuwa akitumia kusafiria kwa passport ya uganda ni Ruwanga Tomas Msisi.
Hongera majeshi ya Tanzania kwa kazi nzuri.Tunawaaminia.
CHANZO: Habari Leo

Kamanda wa waasi wa ADF kurejeshwa Uganda
![]()
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard MembeWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
SERIKALI ya Tanzania inatarajia kumpeleka Uganda Kamanda wa Kikosi cha Waasi cha ADF cha Uganda, Jamil Mukumu aliyekuwa akitafutwa muda mrefu hapa nchini na Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol).
Atapelekwa Uganda baada ya taratibu za kumfikisha mahakamani kukamilika.
"Baada ya kukamatwa mtu huyo tuliwauliza Umoja wa Mataifa kama watamchukua, lakini walikataa njia iliyobaki sasa ilibidi tumfikishe mahakamani na kisha mahakama kwa kufuata sheria ya kubadilishana wafungwa na mahabusu atapelekwa Uganda kwenye mashitaka yake," alisema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Alisema utaratibu huo wa kumpeleka Uganda unafanyika kisheria kwa sababu ndio njia pekee iliyobaki.
Membe alisema pamoja na tukio la wanajeshi wawili kuuawa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na wengine 15 kujeruhiwa, wanajeshi wa Tanzania wanafanya kazi nzuri.
Kundi la waasi la ADF limejikita mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) na limehusika kuua wanajeshi wa Tanzania.
CHANZO: Habari Leo