Kiongozi wa waasi wa ADF-NALU Uganda akamatwa Tanzania na kufikishwa mahakamani

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
3,759
Reaction score
2,206
Kama ilivyo kawaida Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) likianzisha operation yake nje ya nchi lazima lishinde.Likiwa kongo liliweza kuwakimbiza mbio kongo na kuwavurumisha waasi wa M23 ambao wana asili ya Rwanda na kuwatokomoza wasiendelee kuonea wananchi wa kongo.

Safari hii JWTZ inapambana na waasi wa Uganda wa kundi la ADF-NALU kule kongo.ADF-NALU wakajitia wanatikisa kibiriti kwa JWTZ kwa kuushambulia msafara wa JWTZ na kuua askari wawili wa Tanzania.Kilichofuata hapo ni mshike mshike.JWTZ kwa kushirikiana na raia wema,polisi na vyombo vya usalama wamemdaka kiongozi wa kundi hilo Jamil Mukulu na amefikishwa mahakamani Kisutu dar es salaam tarehe 16/05/2015 akiwa chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamevaa nguo za kiraia.Mwasi huyo aliyebadili dini kutoka ukatoliki na kuwa mwislamu jina lake ambalo amekuwa akitumia kusafiria kwa passport ya uganda ni Ruwanga Tomas Msisi.

Hongera majeshi ya Tanzania kwa kazi nzuri.Tunawaaminia.


CHANZO: Habari Leo
 
Jamil Madevu, watu kama hawa ni wa kupotezwa tu, Hongera JWTZ.
 
Muuwaji kama huyo hafai kuishi hongera JWTZ
 
nilimwona huyu jamaa kisutu ijumaaa jana nafikiri. ila nilikuwa sijui kama ni muasi, nilijua ni mtz wa kawaida tu, alikuwa katika ulinzi mkali sana. nilipoangalia picha zake hapa, nimeona yeye mwenyewe kabisa akiwa congo.
 



 
Mtu ana hasi Uganda, anapingana na serikali ya Uganda akitokea congo. Kwanini awaue wakongo? nilitarajia auwe waganda na si wakongo kama kundi lake linavyo fanya. Isije kuwa ni mkono wa mu7 tena kama alivyo wahi kuingia kongo kwa madai ya kuwatafuta waasi
 
Mbona huyu Jamaa yupo nchini Tz siku nyingi hadi na nyumba anazo tena nzuri tu....iweje kundi lake km kweli lifanye maasi nauku yeye akijua yuko Tz? Mie napata wasiwas kidogo hasa tunavyo mfahamu M7 na Kagame wamekua wakifund makundi mengi sana ya kihasi ili kudistabalize DRC na kuiba maliasili kule..Ni ajabu leo hii baada ya tukio UGANDA ndo eti wanamuhitaji huyu tukumbuke pia yule Genaral muasi wa kinyarwanda aliekua akifanya mahasi DRC baada ya kuzidiwa akakimbilia Rwanda na KAGAME mpaka leo halikataa kumpeleka DRC ili ashitakiwe
 
Hongera kwa majeshi yote yaliyofanikisha kukamatwa kwa mpuuzi huyo.
 
Hivi ule usemi wa ukikamatwa ijumaa lazima ulale selo hadi jtatu umekufa siku hizi???

Mahakam inafanya kazi hadi wikiendi.
Sijawahi kuona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…