Kiooo kiooo alikivunja nani, simjui simjui wa mwisho akamatwe atiwe gerezani.....
Huu mti gani wa mchongoma, nikiukata haukatiki, hata kwa shoka haukatiki, hata kwa panga haukatiki, hata kwa jembe haukatiki...........endelea
Sio muda wote mkuu, sisi wengine tunawafundisha nyimbo za enzi za utoto wetu.
-"Sisimizi mwaenda wapi, twaenda msibani, aliyekufa ni nani, aliyekufa mkubwa wetu, kidege zunguruka ukitaka inama inuka".
-Sikiliza mama wee nikwambie hadithi, mikono yangu midogo weee haiwezi kufanya kazi, sikiliza mama wee nitakuwa mkubwa, nitafanya kazi zote nawe (na wewe) upumzike!
Ukuti ukuti, wa mnazi wa mnazi, mwenzetu mwenzetu, kagongwa kagongwa, na gari na gari, tumpeleke mnazi mmoja acje kusema kwa mama yake pyeee pyepye Pye..... Mambo badoooo.......