Kiota cha Ndege

Mrs Kharusy

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
1,244
Reaction score
671
Wapendwa za J1..
Kuna recipe hii ningependa kushare nanyi..

Unga mug 1 na robo
Mtindi plain mug moja
Sukari vijiko 7
Mayai 2
Samli aseel vijiko 4(unaweza tumia mafuta 1/2 mug)
Vanilla 1-2 tbs
Baking powder 2 tbs
Vermicelli 1pkt
Maziwa mazito ya sona kibati 1

Jinsi ya kutayarisha
Kwenye bakuli safi mimina mtindi, mayai, sukari ,samli na vanilla
Tumia mashine ya cake au mchapo kuchanganyia
Then weka unga na baking powder. .changanya vizuri
Kwenye trey weka baking paper na umimine mchanganyiko wako.
vunjavunja tambi zako(Vermicelli) na uziweke juu ya ule mchanganyiko
Bake mchanganyiko wako kwa dkk 25-30
Baada ya kuiva itoe kwenye oven na umimine maziwa ya sona kabla haijapoa
Baada ya kupoa weka kwenye fridge.
Kiota cha ndege tayari kwa kuliwa.
 
Attachments

  • 1400956178485.jpg
    81.7 KB · Views: 332
Hii ndo inaitwa khunafa ama?shogaangu anaitengeneza naipenda dah...lakini si kuna vitambi vyake maalum unatakiwa uvitumie ama?
 
Mie hilo jina lake tu nimelipenda.
Tambi ni lazima ziwe hizo Vermicelli?
 
Hio pic hapo nimeweka step by step..before sijabake..after na baada ya kuitoa kwenye fridge
 
Hii ndo inaitwa khunafa ama?shogaangu anaitengeneza naipenda dah...lakini si kuna vitambi vyake maalum unatakiwa uvitumie ama?
Mimi nimetumia hizi...lkn zozote zinazofanana na hizi unaweza tumia dear
 
Attachments

  • 1400960626765.jpg
    49.8 KB · Views: 124
Mrs Kharusy hiki kiota cha ndege kina jina lingine? Haya sasa weka na mapishi ya jelebi πŸ™‚πŸ™‚ hizi mie nilikuwa nikila moja tu basi siwezi kuongeza, sukari ni nyingi sana na wakati huo wala nilikuwa sijajua madhara ya sukari nyingi mwilini ila zinaweza kutengenezwa kwa labda kuweka sukari kiasi.
 
Last edited by a moderator:

Jelebi km kaimati, bila sukari au sukari kdg hazinogi. Km waogopa sukari bora uachane nazo tu.
 
Last edited by a moderator:
MashAllah, pishi kwa macho tu limeelekea km tamu.

Na kahawa pembeni, Aaah. Mambo mazuri
 
Siogopi sukari kihivyo ila kwenye jelebi naona kama huwa sukari inakuwa nyingi sana, nikila jelebi moja tu basi lakini kuna watu wanaweza kuzila hata tano!!!!

Jelebi km kaimati, bila sukari au sukari kdg hazinogi. Km waogopa sukari bora uachane nazo tu.
 
Jelebi sijakaa kujifunza...kuna wakati fulani mama alikua akitengeneza nzuri lkn sukari ndo hivyo tena km ujuavyo!! ...lol
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Wapendwa za J1..
Kuna recipe hii ningependa kushare nanyi..

....
Bake mchanganyiko wako kwa dkk 25-30
Baada ya kuiva itoe kwenye oven na umimine maziwa ya sona kabla haijapoa
Baada ya kupoa weka kwenye fridge.
Kiota cha ndege tayari kwa kuliwa.

Shukran kwa recipe hii.

Jee temperature iwe ngapi wakati wa kubake?
 
Siogopi sukari kihivyo ila kwenye jelebi naona kama huwa sukari inakuwa nyingi sana, nikila jelebi moja tu basi lakini kuna watu wanaweza kuzila hata tano!!!!

Hapo umesema!!
Ila hivi vyakula vyengine hatupaswi kula kwa kushiba....tule kwa kujiburudisha tu.
Kuhusu jina jengine la huu upishi sina hakika best!!
 
LOL!!!! Na kiota cha ndege kina jina lingine au hilo ndio jina lake halisi?

Jelebi sijakaa kujifunza...kuna wakati fulani mama alikua akitengeneza nzuri lkn sukari ndo hivyo tena km ujuavyo!! ...lol
 
LOL!!!! Na kiota cha ndege kina jina lingine au hilo ndio jina lake halisi?

Mimi naufahamu kwa jina hili..Subiri farkhina aje atuambie yawezekana anaufahamu kwa jina lengine
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…