Kipa wa Man City, Ederson ahamia Fenerbahce ya Uturuki

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Kipa wa Brazil, Ederson, amekamilisha uhamisho wa kudumu kutoka Manchester City kwenda klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ameondoka City baada ya miaka minane, kipindi ambacho aliisaidia timu hiyo kutwaa mataji sita ya Ligi Kuu ya England na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Fenerbahce wamekubaliana kulipa pauni milioni 12.1 kwa kipa huyo ambaye alicheza mechi 372 katika michuano yote akiwa na City, baada ya kusajiliwa kutoka Benfica kwa dau la pauni milioni 35 mwaka 2017.

Wakati huo huo, City wamefikia makubaliano ya pauni milioni 26 kumsajili kipa wa Italia, Gianluigi Donnarumma, kutoka Paris Saint-Germain kwa mkataba wa miaka mitano.

Ederson pia alishinda Kombe la FA mara mbili akiwa na City na akachangia mafanikio ya Pep Guardiola ya kutwaa treble msimu wa 2022-23.

“Ninaondoka Manchester City nikiwa na fahari kubwa kwa kile tulichofanikisha pamoja, na ninaheshimiwa kwa kuvaa jezi hii mara nyingi,” alisema Ederson.

“Chini ya Pep, tumetawala Ligi Kuu na kushinda Ulaya. Imekuwa safari ya kipekee.”

Mbali na kuokoa mabao, Ederson alifanikiwa kuweka clean sheets 122 katika mechi 276 za Ligi Kuu na hata kusajili assist saba kwenye mashindano hayo.

Chanzo: BBC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…