Kipa wa Simba, Ayoub ana mikono mibovu kudaka shuti?

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Simba kwanini wanashindwa kumwamini Salum kama manula hayupo,huyu mwarabu ni mbovu,magoli tuliyofungwa Zambia yote mawili asilimia 70 ni kushindwa kudaka mashuti na asilimia nyingine 30 ni mabeki wa simba.

Kila shuti ikipigwa imo labda kama inaenda nje na unaona ipo chini ya uwezo wa kipa, kama Manula angekuwepo tungekuwa na clean sheet mechi zote mbili. Halafu ana pasi hata za hovyo ,anaweza kutoa pasi mshambuliaji pinzani inampiga kwa kipimo cha kidole gumba,imagine mshambuliaji kama Baleke au Kagere si lazima atoke na goli.

Kipindi Yanga wakiwa ombaomba kipa akiwa kindoki kocha wa makipa alisema Kindoki hafai shuti ikipigwa anafunga macho, mwisho wa siku yeye ndo akafukuzwa.

Hivi Kocha wa Simba haoni mapungufu ya huyo kipa mechi zote?

Robetinho hafai hatua inayofuata
 
Kila shuti ikipigwa imo labda kama inaenda nje na unaona ipo chini ya uwezo wa kipa,
Ina maana leo Power Dynamos wamepiga on target moja tu? Na kule kwao walipiga mbili tu? Huu ndio umaandazi
 
Ina maana leo Power Dynamos wamepiga on target moja tu? Na kule kwao walipiga mbili tu? Huu ndio umaandazi
Sasa kama mi mandazi we si utakuwa chapati
 
Msimtwishe mtoto wa watu matatizo ya timu nzima kiufupi timu nzima ya simba ina matatizo.
Tuache visingizio hilo goli la leo kumlaumu kipa badala ya mabeki walio kuwa wanakabia macho ni ufala.
 
Mu Argentina 🇦🇷 yuko wapi? Mkiona tu mtu ana ngozi nyeupe mnadhani anajua miracle. Mtakuja kumshobokea hadi Deepak Tanna wakati yeye ni mwanamuziki na si mwana soka
 
Manula kashafanya yake anamtia misumari mwarabu ataondoka tu na watampa pesa manula anazotaka
 
kwa hilo goli kipa wa simba hana kosa
 
Wachezaji wa Simba hawajitumi, wanacheza kifaza, hakuna ushindani wa namba Simba ndio maana wachezaji hawajitumi. Inaonekana SIMBA ni timu kubwa kumzidi kocha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…