Kipaji pekee hakitoshi, Elimu ni msingi muhimu katika ukuzaji wa Sanaa

Kipaji pekee hakitoshi, Elimu ni msingi muhimu katika ukuzaji wa Sanaa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Sanaa mara nyingi imekuwa ikitokana na kipaji ambacho msanii anazaliwa nacho, msanii aliyezaliwa na kipaji fulani hufanya vizuri zaidi katika fani husika kwani kitu afanyacho kipo kwenye damu na hufurahia kukifanya. Lakini msanii huyu ili afanye vizuri zaidi anatakiwa kuongezewa elimu katika sanaa husika au elimu ya mambo mbalimbali anuai.

Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana kuacha masomo pale ambapo hujingua na vipaji au husufiwa kwa vipaji walivyonavyo basi huingiwa na kitu naweza kukiita ujinga kwani wengi huona elimu tena haina maana kwa kuwa wanaweza kupata pesa za kuendesha maisha yao na kumiliki vitu vya ndoto zao hivyo elimu si kitu tena ni kupoteza muda.

Ni kweli katika miaka ya hivi karibuni sanaa imewaletea vijana utajiri au kuwaingizia pesa lakini baada ya kupata hizo pesa vijana hao wameonekana wakishindwa kufanya matumizi sahihi ya mali zao au kushindwa kujua kipi cha kufanya ili kutunza pesa wazipatazo kwani wana kiwango kidogo cha elimu.

Wengi wanashindwa kutambua ni namna gani wataingia mikataba mizuri ya kazi zao kwani hawana uwelewa mpana wa mambo. Wengi wameishia kuibiwa kazi zao au kupewa malipo kidogo yakazi zao kwa kuwa walisaini mikataba mibovu ambayo hawakuelewa kuwa ina mitego ya kilaghai. Tumesikia mara nyingi wasanii wakiwatuhumu mameja wao au makampuni nk kuwa wanawaibia au hawawaongozi vyema lakini ukafatilia unakuta sababau kuu ni kiwango chao kidogo cha elimu.

Wasanii wamekuwa ni watu wa kuongea vitu visivyo na tija kwao au kwa jamii kwa kuwa hawana elimu ya kuwaongoza nini wanapaswa kuongea wawapo kwenye jamii au vyombo vya habari, matokeo yake hujikuta wanaongea maneno yoyote tu ili mradi a kujikuta wanaua umaarufu wao.

Lakini wengi wameshindwa kukuza au kuendeleza kazi zao zifike mbalizaidi kwa kuwa hawana mwanga wa nini cha kufanya, wengi hujua kutengeneza kazi lakini kushindwa kuwa wabunifu wa nini kifuate ili kazi zao zifike mbali zaidi. Pia hushindwa kujua waanzie wapi katika kudai haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kulinda au kutetea haki zao ambazo zimepokwa.

Ukiwa na kipaji na elimu hakika utakuwa mbunifu na kazi zako utazibrand vyema na katika ubora wa juu hivyo kuendana ana takwa la soko la kazi yako ndani na nje ya nchi. Elimu kwa wasanii kwa ubora wa kazi zao.
 
Back
Top Bottom