Kipande cha sabuni chafikia Tshs 900

hayaland

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
712
Reaction score
399
Tumezoea sio kawaida sabuni za kawaida zinazokatwa vipande kupanda bei, tumezoea kuwa mche wa sabuni ukipanda sana ni tshs 500/= lakini hadi sasa mche wa sabuni umepanda kutoka shs 2300/= ya mwezi March na kufikia tshs 4000/ kwa mwezi May.

Kipande cha sabuni bei yake ilikuwa ni tshs 500/= na kwa sasa kipande kimefikia tshs 800 hadi 900.

Kwa sasa hakuna kitu hakijapanda BEI. Misumali haijapanda hata shs moja kwa kipindi cha miaka 9, ila kwa kipindi hiki imepanda kutoka 3000 kwa kilo moja hadi tshs 5000 kwa kilo.

Nakumbuka Waziri Mkuu aliwahi kuwaagiza Wakuu wa Wikoa na Wilaya kutembelea masokoni na kwenye maduka ya kawaida ili kuwadhibiti wafanyabiashara wanaopandisha bidhaa holela ila hadi sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa hadi sasa kudhibiti hali hiyo.

Hali sio nzuri sana kwa sasa.
 
Kitafika buku,changamkia fursa ya kutengeneza sabuni
 
Dada ye anasafiri tu hajui uchumi unavyowachumu watu wake huku
 
 

Attachments

  • E7ABC8CA-701E-4822-B7B3-293581B7EC57.jpeg
    25 KB · Views: 13
Waziri mkuu huyu huyu alielaaniwa, Majaliwa alieficha maiti ya Magufuli kituko cha afya Mzena na kwenda msikitini kusema uongo. Mjaalana huyo usimwamini.
Nchi inapitia magumu kwa kua na viongozi HARAMU kama hawa.
 
Maskani kwetu kipande ni buku, tena sio sabuni maarufu kama Jamaa
 
sabuni ya jamaa nayo inaelekea huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…