Kipanya wa leo 26 Febr 2026

Kipanya wa leo 26 Febr 2026

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
1740546353373.jpeg
 
Hiyo 40% ni kodi mpya tena au ndo misada ilio katwa kwenye bajeti yetu ya mwaka?

Ila kama ni msaada ambao ulikua una saidia annual bajeti ya nchi, serikali ina wigo mpàna wa kupinguza matimizi ya sio ya lazima kupata hizo pesa, futeni vyeo visio muhimu, kama mkuu wa wilaya, naibu waziri, magari ya kifahari nk.
 
Hawanaga akili ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali wanachowaza wao ni namna Gani ya kumkamua mwananchi zaidi kunenepesha matumbo Yao
 
Punguzeni ukubwa wa baraza la mawaziri, punguzeni utitili wa manaibu Waziri, magari ya kifahari serikalini yawekewe mwongozo wa nani na nani atumie gari lipi. Magari kwenye msafara yapunguzwe kwa Rais yasizidi magari 10. Waziri mkuu magari 5. Punguza saana safari za nje ya nchi. Kwa sasa hivi Rais ana kwenda nje ya nchi kwa wastani wa Mara moja kila Mwezi. Hii si sawa. Na safari moja Inakula kwenye sh billion.
 
Hali itawalazomisha wewe huoni ma graduate hawana ajira utalipaje kodi, watu kila siku wanakua masikini nani alipe kodi uchumi umeduma tu.
 
Hiyo 40% ni kodi mpya tena au ndo misada ilio katwa kwenye bajeti yetu ya mwaka?

Ila kama ni msaada ambao ulikua una saidia annual bajeti ya nchi, serikali ina wigo mpàna wa kupinguza matimizi ya sio ya lazima kupata hizo pesa, futeni vyeo visio muhimu, kama mkuu wa wilaya, naibu waziri, magari ya kifahari nk.
Hapo hawatafanya hivyo.
 
Samia na genge lake akili yao yote iko kwenye uchaguzi!!
Hawa jamaa ili kubalance budget yao akili yao kila siku ni kuongeza mapato kwa kuwakamua wananchi badala ya kuangalia jinsi ya kupunguza matumizi yao!! Samia kuwa na baraza kubwa la mawaziri sio ishara ya ufanisi. Kwa nchi masikini, that is extravagance bibi. Punguza ukubwa wa baraza hali ya kiuchumi ni tete.
 
Samia na genge lake akili yao yote iko kwenye uchaguzi!!
Hawa jamaa ili kubalance budget yao akili yao kila siku ni kuongeza mapato kwa kuwakamua wananchi badala ya kuangalia jinsi ya kupunguza matumizi yao!! Samia kuwa na baraza kubwa la mawaziri sio ishara ya ufanisi. Kwa nchi masikini, that is extravagance bibi. Punguza ukubwa wa baraza hali ya kiuchumi ni tete.
Punguzeni ukubwa wa baraza la mawaziri, punguzeni utitili wa manaibu Waziri, magari ya kifahari serikalini yawekewe mwongozo wa nani na nani atumie gari lipi. Magari kwenye msafara yapunguzwe kwa Rais yasizidi magari 10. Waziri mkuu magari 5. Punguza saana safari za nje ya nchi. Kwa sasa hivi Rais ana kwenda nje ya nchi kwa wastani wa Mara moja kila Mwezi. Hii si sawa. Na safari moja Inakula kwenye sh billion.
Lakini kwa akili za watawala wetu utakuta bado wanashindana kununua mashangingi ya serikali
Hiyo 40% ni kodi mpya tena au ndo misada ilio katwa kwenye bajeti yetu ya mwaka?

Ila kama ni msaada ambao ulikua una saidia annual bajeti ya nchi, serikali ina wigo mpàna wa kupinguza matimizi ya sio ya lazima kupata hizo pesa, futeni vyeo visio muhimu, kama mkuu wa wilaya, naibu waziri, magari ya kifahari nk.

Watawala wa nchi hii ni lazima wakubali kubadilika, Sera ya Mpango wa Kubana Matumizi ya Serikali kwa Sasa haiepukiki. Tutake tusitake, ni lazima Muundo wote kabisa wa Utendaji wa Serikali unapaswa kubadilisha na kufanya Mass Redundancy kwa Watumishi wa Umma.

Watumishi wa Serikali wengi sana wanapaswa kupunguzwa kazi angalau kwa asilimia hamsini wakibakizwa wale tu ambao ni lazima wawepo kama vile Madaktari wa Tiba ya binadamu na mifugo, manesi, pamoja na Sekta zingine muhimu zaidi.

Taasisi nyingi sana za Serikali zinapaswa kufutwa Kabisa kutoka katika Muundo wa Serikali, sambamba na kufuta Vyeo vingi visivyokuwa na UMUHIMU wowote ule katika nchi hii.
Taasisi hizo na Vyeo ambavyo vinapaswa kufutwa ni kama ifuatavyo, hii ni kutokana na maoni yangu binafsi:-
1. Sekretarieti zote kabisa za Mikoa zinapaswa kufutwa zote. Badala yake Halmashauri za Wilaya, Miji, na Majiji ndizo zinapaswa kubakizwa.

2. Vyeo vya Wakuu wa Mikoa(RC), RPC, RSO, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS) na wa Wilaya (DAS), n.k, vinapaswa kufutwa kabisa.

3. Taasisi zingine za ajabu ajabu huko Serikalini pia zinapaswa kufutwa. Kwa mfano kama vile sijui Taasisi ya Mbolea, Bodi za Mazao kama vile Pareto, Karafuu, Pamba, sijui bodi ya mazao ya Michikichi, n.k, Zote hizi ni za kuzufutilia mbali kabisa.
 
Ma Vx V8 yote serikali iache kununua kabisa, Land Cruiser Prado inatsosha sana kuanzia kwa Manaibu Waziri, Wakuu wa Mikoa, Na maafisa wengine wa Serikali..

Vx V8 zibakie kwa Mh. Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Makamu Waziri Mkuu na Mawaziri tu..!! Hii itapunguza sanaa matumizi ya Serikali
 
Back
Top Bottom