Samia na genge lake akili yao yote iko kwenye uchaguzi!!
Hawa jamaa ili kubalance budget yao akili yao kila siku ni kuongeza mapato kwa kuwakamua wananchi badala ya kuangalia jinsi ya kupunguza matumizi yao!! Samia kuwa na baraza kubwa la mawaziri sio ishara ya ufanisi. Kwa nchi masikini, that is extravagance bibi. Punguza ukubwa wa baraza hali ya kiuchumi ni tete.
Punguzeni ukubwa wa baraza la mawaziri, punguzeni utitili wa manaibu Waziri, magari ya kifahari serikalini yawekewe mwongozo wa nani na nani atumie gari lipi. Magari kwenye msafara yapunguzwe kwa Rais yasizidi magari 10. Waziri mkuu magari 5. Punguza saana safari za nje ya nchi. Kwa sasa hivi Rais ana kwenda nje ya nchi kwa wastani wa Mara moja kila Mwezi. Hii si sawa. Na safari moja Inakula kwenye sh billion.
Lakini kwa akili za watawala wetu utakuta bado wanashindana kununua mashangingi ya serikali
Hiyo 40% ni kodi mpya tena au ndo misada ilio katwa kwenye bajeti yetu ya mwaka?
Ila kama ni msaada ambao ulikua una saidia annual bajeti ya nchi, serikali ina wigo mpΓ na wa kupinguza matimizi ya sio ya lazima kupata hizo pesa, futeni vyeo visio muhimu, kama mkuu wa wilaya, naibu waziri, magari ya kifahari nk.
Watawala wa nchi hii ni lazima wakubali kubadilika, Sera ya Mpango wa Kubana Matumizi ya Serikali kwa Sasa haiepukiki. Tutake tusitake, ni lazima Muundo wote kabisa wa Utendaji wa Serikali unapaswa kubadilisha na kufanya Mass Redundancy kwa Watumishi wa Umma.
Watumishi wa Serikali wengi sana wanapaswa kupunguzwa kazi angalau kwa asilimia hamsini wakibakizwa wale tu ambao ni lazima wawepo kama vile Madaktari wa Tiba ya binadamu na mifugo, manesi, pamoja na Sekta zingine muhimu zaidi.
Taasisi nyingi sana za Serikali zinapaswa kufutwa Kabisa kutoka katika Muundo wa Serikali, sambamba na kufuta Vyeo vingi visivyokuwa na UMUHIMU wowote ule katika nchi hii.
Taasisi hizo na Vyeo ambavyo vinapaswa kufutwa ni kama ifuatavyo, hii ni kutokana na maoni yangu binafsi:-
1. Sekretarieti zote kabisa za Mikoa zinapaswa kufutwa zote. Badala yake Halmashauri za Wilaya, Miji, na Majiji ndizo zinapaswa kubakizwa.
2. Vyeo vya Wakuu wa Mikoa(RC), RPC, RSO, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS) na wa Wilaya (DAS), n.k, vinapaswa kufutwa kabisa.
3. Taasisi zingine za ajabu ajabu huko Serikalini pia zinapaswa kufutwa. Kwa mfano kama vile sijui Taasisi ya Mbolea, Bodi za Mazao kama vile Pareto, Karafuu, Pamba, sijui bodi ya mazao ya Michikichi, n.k, Zote hizi ni za kuzufutilia mbali kabisa.