Ibun Sirin
Member
- May 20, 2022
- 50
- 106
Huu ni moja ya uchawi hatari sana, ni uchawi unaofanywa kwa malengo maalum na kwa muda maalum, kipapai ni kuzubaishwa au kuangamizwa na kudhurika kimwili na kiakili, kuna kipapai cha kumfanya hakimu kupindisha hukumu, kwa kifupi haya ni matukio ya kupumbaza akili na kuja kushtuka baadae mambo yanapokuwa yamekwisha, kuna kipapai cha maradhi mfano wa kiharusi pia kuna kipapai cha kwenda hovyo n.k.
Imeitwa kipapai kwasababu inavuruga akili mfano wa mbegu za papai zinavyo vurugika ukizipukuchua, pia mtendaji wa hili hupaka dawa ambayo hupelekea mikono kuwa mieusi mfano wa mbegu za papai.
Imeitwa kipapai kwasababu inavuruga akili mfano wa mbegu za papai zinavyo vurugika ukizipukuchua, pia mtendaji wa hili hupaka dawa ambayo hupelekea mikono kuwa mieusi mfano wa mbegu za papai.