Kipato Cha Diamond Platinumz, Je Wajua Analipwa Ngapi Kufanya Shoo Moja?!?

Ibrahim300

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
390
Reaction score
68
Bila shaka msanii huyu anayetamba sahizi kwa nyimbo yake mpya ya My Number One remix ni staa wa kulengwa kwa manati.

Diamond Platinumz kwa sasa yupo na anazidi kuendelea kuwepo kila uchao. Staa huyu anayegonga vichwa vya habari kila siku amedhihirisha kuwa ameweza kuistadi tasnia ya mziki na kuijua nje na ndani jinsi ya kufanikisha mziki na umaarufu wake.

Platinumz ni msanii anayemiliki pesa nyingi, dhihirisho lake moja ni thamani ya video yake mpya ya My Number One Remix na nyingine jumba analolijenga sahizi na pia bling zake za dhahabu.

Lakini je msanii huyu pesa zake huzitoa wapi?

Usanii hulipa bora tu uwe mjanja. Kulingana na mwanahabari mwenye uhusiano wa karibu na mastaa wengi, Willy M Tuva, mwendeshaji wa kipindi cha muziki wa kizazi kipya nchini Kenya amebainisha kuwa Diamond ni mfano wa matawi ya juu.

Tuva alibainisha kuwa kama unataka kumkodisha Diamond aje akufanyie shoo usiku mmoja lazima uwe na dola $20,000. Diamond atagharamia mengineyo kama dansa, uchukuzi nk.

Hizi ukizijeuza pesa za kibongo ni takriban milioni 32,000,000 usiku mmoja pekee...kiufupi Diamond ameonyesha kuwa ataendelea kuwakandamiza wasanii wenzake kwa upande wa mashabiki, umaarufu na.....kimkwanja.

Nani alisema mziki hauna faida?

Chanzo: Kipato Cha Diamond Platinumz, Je Wajua Analipwa Ngapi Kufanya Shoo Moja?!? - bkuHABARI
 
Hizo million 32 ukimpa akapiga Dar live peke yake kwa kiingilio cha shillingi @10,000. Sawa na watu 3200 waingie Dar live. Haya niambie hawa watu 3200 utawapata? Kumbuka watoto ni Tshs @5000 utawapata? Haya gharama za maandalizi, promotion faida nk. TUSIDANGANYANE sisi ni watu wazima.
 

Wewe unalipwa shillingi ngapi?
 

nimeshasema toka mwaka huu uanze, mtu yeyote atakae comment point ikanigusa kwenye mtima, sinto toa LIKE ila badala yake ntatoa vocha ya elfu mbili, weka namba yako uchukue vocha yako fasta
 

Hizo pesa hazitoki kwa watu pekee bali pia kwa wahisani kadhaa...mfano Diamond atake kupiga shoo Dar Live halafu Vodacom wajitokeze, wataka kuniambia watapewa promo bure?
 
nimeshasema toka mwaka huu uanze, mtu yeyote atakae comment point ikanigusa kwenye mtima, sinto toa LIKE ila badala yake ntatoa vocha ya elfu mbili, weka namba yako uchukue vocha yako fasta

Kabla hujatoa vocha hebu jaribu kuwaza kama anaongea ukweli, ama utafiti wake ameufanya wapi na nani
 

Badala kuwaza yako,,, hovyo ukijua halafu
 
Analipwa ml 10 tu kwa shoo chanZo yy mwenyewe

Hiko chanzo kimetoka kwa mwanahabari wa Kenya Willy M Tuva, hua ana kipindi cha mambo mseto katika runinga ya Citizen...inamaanisha akipiga shoo nje anapata hizo pesa

Jamaa mbona muna bifu za kijinga na wasanii ama mwalipwa kumkandamiza Diamond? Kama nyinyi hamumtaki Diamond bana Nigeria washamkubali(internationale)
 
Siamini badoo unavyompambaa maana hajamfikiaa, ,
Hiv Davido ni msanii mkubwaaa sanaa duniani?????
 
Hizo pesa hazitoki kwa watu pekee bali pia kwa wahisani kadhaa...mfano Diamond atake kupiga shoo Dar Live halafu Vodacom wajitokeze, wataka kuniambia watapewa promo bure?

Hapa tunaongelea show zinAzosimamiwa na mapromotor, hayana udhamini wa Vodacom wala Airtel au chochote, na promota anagharamia nauri na madancer wake, hotel na chakula, alipie ukumbi, wasimamizi mabaunsa nae apate faida, itatoka wapi? Pia show show ya mwimbaji mmoja hainogi inabidi uwachanganye ma artists kama watatu au wanne, ndiyo inakuwa kivutio nao walipwe! Hao waongo wanalipwa ml 10 au 15 tu!
 
Inahusu nini kipato chake. Du bongo bwana ajiandae na majambazi kawatangazia deal
 
Kule kwenye jukwaa la siasa kuna wanasiasa wameajiri vijana kwa ajili ya kupost habari zao tu,kumbe huku pia yapo,diamond kaajili watu kua wanapost habari zake tu,haipiti saa 1 utaona post inayomhusu diamond,iktokea bahat mbaya akafa cjui mtapata wap za kupost,mtakufa njaa,fanyen kaz zngne
 

Siku za hivi karibun ilishawahi kusemwa kuwa ili huyo Naseeb apige show anataka Tsh 10m/-. Na kwa kweli ni uongo kusema wafadhili watamlipa ukumbini, labda kwenye tamasha la wazi. Hivyo hiyo 32m/- labda kwa huko Kenya. Unajua tunapenda kukuza sana mambo. Yafaa tumpongeze mdogo wetu Naseeb, kwa ubunifu wake ambao unampa kipato, lakini siyo kama tunavyoaminishwa kwa kiasi kikubwa
 
Tangia msanii mmoja ajipambambanue kuwa lijiumba la milioni 200 ni lake, halafu ghafla mwenye nyumba kagoma kuendelea kumpangisha, kampa notice siwaamini kabisa hawa watu wa hii tasnia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…