KIPAUMBELE CHETU KWA SASA KAMA TAIFA NI KIPI?

KIPAUMBELE CHETU KWA SASA KAMA TAIFA NI KIPI?

klementos

Senior Member
Joined
Aug 29, 2017
Posts
105
Reaction score
757
Toka tunapata uhuru 1961 kipaumbele chetu kama taifa ni Kilimo. Kauli mbiu kubwa ilikuwa ni kilimo ni uti wa mgongo, hadi sasa japo ni lugha tu ya mdomoni hila hatuitendei haki kauli hii.
Kwa mujibu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu za 2012, kilimo kinachangia 24.7% ya pato la taifa na pia kilimo kinachangia 74% ya fedha za kigeni. Kitu kikubwa kinachofanya kilimo kisifanye vizuri ni kwa sababu ya kutegemea mvua, kupelekea watu wengi kuogopa kufanya uwekezaji na kuwaachia watu wa Vijijini.

Kuna ulazima wa kuweka kipaumbele cha ujenzi wa Irrigation scheme Tanzania, kwenye kila Wilaya ambazo hazipati mvua zakutosha kwa mwaka. Tanzania kipindi cha mvua maji mengi sana yanapotea. Kama Serikali itaweza kuja na mpango mkakati wa wa kukusanya maji yanayopotea kipindi cha mvua kwa kuyajengea Schemes na wananchi wakafanya Kilimo cha umwagiliaji, Taifa litaondokana kwa kiasi kikubwa na tatizo la njaa, tatizo la kupanda kwa bei ya vyakula kila mwaka na pia taifa litapata fedha nyingi za kigeni.

Wataalamu wanasema gharama ya ujenzi Irrigation Scheme USD 4,800-5,500/Hactare hususani kwenye nchi zetu za Kiafrica. Kwa kiasi nadhani hatuwezi kushindwa kama Taifa kulingaisha na miradi mingi inayotekelezwa kwa sasa .

Tunaweza jiwekea mpango mkakati wa miaka 5-10 kufanikisha miradi ya umwagiliaji ambayo itamgusa mtu wa chini kabisa na kumkomboa toka kwenye umaskini mkubwa kuliko kujikita kwenye miiradi mikubwa isiyomgusa moja kwa moja yule mtu wa chini ambae japo anaweezeshwa kwa kiwango cha chini ila anasaidia kama Taifa kupata fedha za kigeni 74% na kuchangia pato la Taifa 24%. Je akiwezeshwa?
 
Pamoja na hayo ya wanaotegemea mvua za msimu lakini bado soko haliko rafiki kwa mkulima!
Mkakati wa uboreshaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji iendane sambamba na utafutaji wa masoko ya ndani na ya nje.
 
Binafsi siamini kama Nchi ina kipau mbele kwani kuna vitu kama vitatu naona vinapiganiwa sana na Viongozi wetu navyo ni Viwanda, Makusanyo ya Kodi na Miundo mbinu sasa sijui kipau mbele ni kipi hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi siamini kama Nchi ina kipau mbele kwani kuna vitu kama vitatu naona vinapiganiwa sana na Viongozi wetu navyo ni Viwanda, Makusanyo ya Kodi na Miundo mbinu sasa sijui kipau mbele ni kipi hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Viwanda vingi vinajengwa mjini, Kijijini ni 0.1% na huko vijijini wengi ni Unskilled labor hawezi kupata ajira na pia Vijiji vichache sana vina miundo mbinu. Miundo mbinu ya umwagiliaji itawawezesha walio vijijini nao kushiriki kula keki ya taifa angalau kwa kiasi kidogo.
 
Kununua wapinzani tu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom