Thanks Dyslexia
Pole Susy,nenda kafanye uchunguzi,yaweza kuwa warts,wanakata tu na kuchoma,mzigo unakuondoka.Kama uko dar nenda Tumaini Hospital!
Nawasalimuni nyote!!
Wapendwa nina zaidi ya miaka nane nina kipele kidogo sana mfano wa chunusi ambacho mpaka nijishike mwenyewe ndio nijue kama kuna kipele. Kipele hicho nimekaanacho takribani ss miaka 8, hapo awali sikudhani kama ni shida na niliona ni hali tu ya kawaida, ila kwa ss nasikia kama kinavuta, nimekwenda hospitali nimepewa dawa mbali mbali, mpk ss nimechoka maana kila niikieenda hospitali mpaka nimtanulie dr. anitie vidole naye aangalie.
Naombeni msaada wenu.
Nanren
Ni ndani kabisa ya uke, na mpaka uingize kidole cha kati kiingie nusu ndio unaweza kukikuta, na kilinipata miaka 8 iliyopita ambapo sikujua maana hata ya kujisafisha sanaa kama ss nilivyo, hakiumi hata kidogo, hata siwezi wakati mwingine kuhisi kama ninakipele mpaka wakati nanawa, ila ss nimeanza kukisikia kama kinavuta mara moja moja kama vile ni ganzi fulani, yaani sijui nikueleezee vipi unielewe, lakini natumai umenisoma.
Zaidi ya yote nashukuru kwa ushauri wako nitaufanyia kazi, be blessed
Nawasalimuni nyote!!
Wapendwa nina zaidi ya miaka nane nina kipele kidogo sana mfano wa chunusi ambacho mpaka nijishike mwenyewe ndio nijue kama kuna kipele. Kipele hicho nimekaanacho takribani ss miaka 8, hapo awali sikudhani kama ni shida na niliona ni hali tu ya kawaida, ila kwa ss nasikia kama kinavuta, nimekwenda hospitali nimepewa dawa mbali mbali, mpk ss nimechoka maana kila niikieenda hospitali mpaka nimtanulie dr. anitie vidole naye aangalie.
Naombeni msaada wenu.
Suzy Pole, nimesoma ushauri wa watu mbali mbali, kila mtu anafikiri kivyake na hiyo ndio medicine, u can have a lot of differential diagnoses.
Mimi sidhani sana kama ni Bartholin's cyst kwa kuwa yenyewe usingekaa nayo for 8 years, lazima ingekusumbua na pia hiyo cyst huwa haiko ndani sana huwa kama 0.5 to 1cm inside the vagina from the introitus, na ile huwa inakuwa with time, na huweza kukua na hata kuonekana imevimbe kwa nje kwenye labium majus.
Umewahi kushika Cervix yako? Nimeshawahi kupata complaint ya mtu akidai ana uvimbe ndani ukeni lakini ilikuwa ni cervix, alipoigusa kwa mara ya kwanza akajua ni uvimbe. Jaribu kujichunguza vizuri some people do confuse the cervix with a mass or a nodule na utajicheka ukigundua hicho unachodhani ni kijipele kikajakuwa ni maumbile yako ya kawaida.
Sidhani pia kama ni warts kwani zenyewe mara nyingi huwa zinakuwa nje zaidi kwenye perineum kuliko ndani unless ziwe very extensive. Na huwa zinakuwa na feel fulani rough unapokashika sijui zako zikoje. Ni kweli Warts zinasababishwa na virusi aina ya HPV type 6 and 11 in 90% of patients, virusi hivi havisababishi cancer, vinavyosababisha cancer ni virusi vya HPV type 16 and 18 and others ambavyo vinasababisha cervical cancer, kwa hiyo hata kama ni warts usihofu haiwezi kuwa cancer baadaaye.
Daktari aliyekupa dawa alikwambia shida ni nini? Kama unawasiwasi sana u better see a gynaecologist atakutoa huo wasiwasi