Kipengele gani cha Katiba ya Tanzania kinachopiga marufuku uraia pacha?

Ni sehemu gani katika Katiba ya Tanzania inaposema ukiwa raia Mtanzania ukachukua uraia wa nchi nyingine unakuwa umepoteza uraia wa Tanzania?
Sio kila kitu kimeandikwa kwenye katiba, vitu vingine ni kwenye sheria taratibu na kanuni。

Kwavile Tanzania hatuna uraia pacha, Raia wa Tanzania akipewa uraia wa nchi nyingine yoyote kwasababu yoyote, atahesabika ameukana uraia wake wa Tanzania hivyo anapokonywa Utanzania wake!

Sheria hiyo ya uraia ni miongoni mwa sheria batili kinyume na katiba, kwasababu uraia wa kuzaliwa ni haki ya msingi ya mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania na haiwezi kuondolewa na mamlaka yeyote, kama ilivyo the right to life, lakini sheria zetu zinasheria batili ya hukumu ya kifo。

More karibu
P
 
Sheria, taratibu au kanuni gani zilizotungwa na bunge au idara ya uhamiaji kufafanua au kutoa muongozo katika suala la uraia pacha? Kama zipo hizo sheria na kanuni ziweke hapa tafadhali.
Au kwa maana nyingine Mtanzanja akichukua uraia wa nchi nyingine atapoteza uraia wake kwa sheria au kanuni gani?

Hata Marekani katiba na sheria zao hazizungumzii kabisa uraia pacha ila raia wa Marekani hawapotezi uraia wao kwa kuwa na uraia wa nchi nyingine!
 
Sheria ya Uraia ya Tanzania ya mwaka 1995 Sura 357 kama ilivyorejewa mwaka 2002, pamoja na kanuni zake za mwaka 1997.
P
 
Sheria ya Uraia ya Tanzania ya mwaka 1995 Sura 357 kama ilivyorejewa mwaka 2002, pamoja na kanuni zake za mwaka 1997.
P
Wenzetu wanatumia ILANI ya chama, chochote wasichokitaka wao kinaundiwa kanuni.
Swali, hadhi maalumu iko kwenye sehemu gani ya sheria hiyo ya uraia ya mwaka 1995?
Inapigiwa debe, je ni sahihi kisheria?
 
Ni sehemu gani katika Katiba ya Tanzania inaposema ukiwa raia Mtanzania ukachukua uraia wa nchi nyingine unakuwa umepoteza uraia wa Tanzania?
Ili nchi hiyo nyingine ikupe uraia wa nchi yao unalazimika kuukataa (denounce) huo uraia wa nchi ulikotoka. Kwa hiyo hao waliokuwa watanzania walio na uraia wa nchi nyingine walishaukataa uraia wao wa Tanzania. Walishaupa taraka utanzania wao, wakachukua wa mwingine.

Ni kama ilivyo kwenye ndoa. Wamebaki kuwa ex wetu. They're Ex-Tanzanians. Tunawapenda na siku wakiamua kumwacha huyo mwingine (kuuacha uraia wake) na kurudi kwetu, uraia wao wa Tanzania utarejea. Huu ndiyo msingi wa sheria zetu kuhusu watu hao walioshaukana uraia wa Tanzania. Hawawezi kuja kugombea au kuteuliwa kwenye nafasi za uongozi wa nchi hususani ubunge, uwaziri, uraisi au kufanya kazi kwenye majeshi yetu au kwenye taasisi zetu nyeti wakati wao pia wana uraia wa nchi nyingine. Ila kama ex wetu sheria zetu zinawapa priority ya juu (versus other foreigners) kuwekeza, kufanya biashara na mambo mengine mbali mbali katika nchi yetu kwani ndiyo motherland yao. Tumewapa special privileges hawa ex wetu. Yote haya ni kwa ajili ya usalama wa nchi yetu. The national security of our nation is of paramount importance.
 
kama jibu ni kwamba hakuna kipengele cha katiba , hao wanaotunga sheria ambazo ni kinyume na matakwa ya katiba wanachukuliwa hatua gani kwa ku- act " ultra vires"? - beyond the scope of their authorities?
 
Ni sehemu gani katika Katiba ya Tanzania inaposema ukiwa raia Mtanzania ukachukua uraia wa nchi nyingine unakuwa umepoteza uraia wa Tanzania?
Kiukweli kipengele wanachokitumia ni kwamba ukiwa raia wa Tanzania huwezi kuwa Raia wa nchi nyingine, hivyo ukichukua uraia wa nchi nyingine automatically unapoteza uraia wa Tanzania. Hakuna sehemu yoyote unaenda kuukana uraia wa Tanzania.
 
Ni sehemu gani katika Katiba ya Tanzania inaposema ukiwa raia Mtanzania ukachukua uraia wa nchi nyingine unakuwa umepoteza uraia wa Tanzania?
Tatizo sisi kila taasisi ina sheria zake kwa ajili ya maslahi yake na watu wachache,ila ukichunguza utakuta sheria mama ambayo ni Katiba yetu ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania haitambui hizo sheria gandamizi ambazo zinakiuka misingi ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
 
Kiukweli kipengele wanachokitumia ni kwamba ukiwa raia wa Tanzania huwezi kuwa Raia wa nchi nyingine, hivyo ukichukua uraia wa nchi nyingine automatically unapoteza uraia wa Tanzania. Hakuna sehemu yoyote unaenda kuukana uraia wa Tanzania.
Ikiwa mtu amezaliwa Marekani na wazazi wote wawili ambao ni raia wa Tanzania halazimiki kuukana uraia wa Marekani ili atambulike kuwa raia wa Tanzania?
 
Ikiwa mtu amezaliwa Marekani na wazazi wote wawili ambao ni raia wa Tanzania halazimiki kuukana uraia wa Marekani ili atambulike kuwa raia wa Tanzania?
Una hoja nzuri zenye mashiko ambazo zinaumiza baadhi ya watu.
 
Ninachojua mimi serikali yaa CCM na watu wake ndiyo kikwazo namba 1 cha uraia pacha. Na ukiwauliza sidhani kama wana sababu za msingi za kuzuia uwepo wa uraia pacha kama ilivyo kwa baadhi ya nchi nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…