Kipengere gani umekipenda au hujakipenda katika rasimu ya katiba iliyozinduliwa leo!

Kipengere gani umekipenda au hujakipenda katika rasimu ya katiba iliyozinduliwa leo!

Rais kumteua jaji mkuu, mwanasheria mkuu, mkuu wa polisi na msajili wa vyama vya siasa
 
Kwa sasa tuna jumla ya majmbo mangapi? Na yatapunguzwaje mpaka yafkie 50 kwa TZ bara? Naomba jbu jaman...
 
Kwa sasa tuna jumla ya majmbo mangapi? Na yatapunguzwaje mpaka yafkie 50 kwa TZ bara? Naomba jbu jaman...

Siyo hayo majimbo ya sasa,ni mjimbo yatakayotoa wawakilishi wa muungano tu.(wabunge wa muungano)
 
Hakuna hatima ya katiba ya tanganyika,na haijulikani ni lini watakuja kuanzisha mujadala huo.
 
Hakuna hatima ya katiba ya tanganyika,na haijulikani ni lini watakuja kuanzisha mujadala huo.

ki ukweli mimi ni muumin wa Muungano achilia mbali huu wa Tanganyika na Zanzibar pia nataman Afrika nzima kuwa nchi moja hivyo sipendi kusikia rasim hii kutaja raisi waTanganyika!! Nataman ingesema tuwe na rais mmoja tuu, wa JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA na zanzibar iwe mko tu itakayokuwa chini ya mkuu wa mkoa tu! ... Tanganyika ni kitu gani?? Aliyesema Tanganyika inaanzia hapa na inaishia hapa ni nan??... Tunafaham alikuwa na malengo gani??... Na kwanini aseme hii itaitwa Tanganyika, hii Zanzibar, ile Burundi, kule pataitwa Malawi... N.k., TUIRUDIE AFRIKA ILIYOKUWEPO KABLA YA MKOLONI!
 
Nimekipenda kipengele kilichosema Mahakama ya kadhi inaweza kuanzishwa hata bila ya kuwemo kwenye katiba. Kuna watu walipigania sana hii mahakama iingizwe kwenye katiba ili serikali iwe inawalipa hela za bure, lakini inabidi wamlaumu aliyewaahidi kuiunda kwenye uchaguzi wa 2005 halafu akaifuta ahadi kimya kimya kwenye uchaguzi wa 2010
 
Rasimu hii imejikita zaidi kwenye muungano tu, vitu vingi vya msingi wameviacha, ina maana baada ya hii tunaanza mchakato wa katiba ya Tanganyika?
 
Nimependa Tanzania Bara kuwa na Majimbo 50 na kila jimbo kuwa na wabunge wawili tu.
 
-NISINGEPENDA Rais kumiliki ardhi, ardhi iwe ni mali ya watanzania (Mwananchi mmoja mmoja), kama kuna matumizi ya kitaifa serikali ilinunue na kumpatia eneo jingine mtu huyo.

-Raisi ASITEUWE Jaji Mkuu, kuwepo na chombo kitakacho msaili mwombaji ambaye tathibitishwa na Bunge. Muhimili wa Sheria ujitegemee kabisa na Rais asiwe na amri kwayo.

-Mwanasheria Mkuu asiteuliwe na Rais, iwe ni ajira itakayo thibitishwa na Bunge.

-Vyeo vya Wakuu wa Mikoa viondolewe na kuwe na Magavana wa kuchaguliwa na wananchi.

-Wakuu wa Wilaya waondolewe kubaki na Mkurugenzi wa Maendeleo aliye ajiriwa na Halmashauri za Wilaya atawajibika kwa Baraza la Madiwani.

-Wakuu wa Idara wilayani waajiliwe na Halmashauri na wawajibike kwa Baraza la Madiwani.
 
Nimeipenda mawazir kutokuwa wabunge sasa siasa zimeisha mawizaran wataalam watapata nafasi kutekeleza mipango ya maendeleo
 
16(1) Kuhusu kutangaza mali kwa mtumishi wa Umma; napendekeza kuwa Kiongozi wa Umma atangaze mali na thamani siku 30 kabla ya kuwa kiongozi na wali SI siku thelethini baada ya kuwa kiongozi. Hii maana yake kama kuna mtu mwenye hoja za ya msingi ya kupinga uhalisia/ufichaji wa mali/thamani ya mtumishi mtarajiwa aweze kuwasilisha pingamizi au hoja, kwani kutaja mali baada ya kuwa kiongozi kutaleta tabu ya kumvua madaraka au gharama za kumvua madaraka pindipo ikibainika kwamba kiongozi huyo alitangaza mali/thamani zake kiuongo isivyo kweli/. Ikumbukwe hapa lengo si tu kutangaza kama ilivyo sasa bali pia uchunguzi ufanyike wa kubaini uhalisia na uhalali wa mali hizo/thamani na ikiwa amezipata kihalali au kimagendo, na pia atangaze kama ni mfanyabiashara na atangaze biashara zake na awe tayari kupitia kampuni yake kukaguliwa hesabu za biashara yake ili mwisho wa siku tujue thamani ya mali zake baada ya kutumikia uongozi zinaendana na chumo lake. Tukifanya hivi tutapata viongozi ambao kweli wazalendo kwani wasio wazalendo wataogopa wakijua kuwa mwisho wa kubainika kwa uongo wao ni confiscation ya mali zake. Pliiiiiiiiiiiz; Lakini akishaingia katika uongozi atalindwa na sheria nyingi za uongozi na ugumu wa kufanyiwa assessment ya haki. Hata hivyo hii natumaini kuwa kifungu hiki kitawagusa watumishi ambao ni highly personnel, hivyo kuteuliwa/kuchaguliwa kwao kazini hakutakuwa na haraka na hakutazuia watanzania wengine wasijue wamuhoji kama si muadilifu
 
Nimependa hapa m bunge anapovurunda wapigakura wamfukuze ubunge. hapa wengi itabidi watoke dsm warudi kujenga majimboni mwao mana ht nyumba, walijengea dsm
 
Mshindi wa urais lazima apate zaid ya kula 50%.....apa tunakaribisha upotevu wa amani na gharama zisizo za msingi mie bdo napendelea mwenye kula nyingi zaid ya wenzake achukue nchi
 
Hakuna sababu yoyote ya jimbo moja kuwa na wabunge wawili. hii ni kuongeza mzigo kwa watanzania.
 
Sijapenda vipengere vyote vinavyotumia kikundi nomino 'Tanzania Bara' badala ya nomino 'Tanganyika'. Hivi jina 'Tanganyika' limefanya nini hadi lichukiwe hivi? Nimepitia rasimu yote nomino 'Tanganyika' imeonekana mara 8 tu wakati kN 'Tanzania Bara' kimeoneka mara 46. Wakati umefika tuelezwe jina Tanganyika lina udini, ukabila, urangi kiasi cha kuchukiwa hivi? Mbona Zanzibar wanaendelea kutumia jina lao!
 
Back
Top Bottom