-NISINGEPENDA Rais kumiliki ardhi, ardhi iwe ni mali ya watanzania (Mwananchi mmoja mmoja), kama kuna matumizi ya kitaifa serikali ilinunue na kumpatia eneo jingine mtu huyo.
-Raisi ASITEUWE Jaji Mkuu, kuwepo na chombo kitakacho msaili mwombaji ambaye tathibitishwa na Bunge. Muhimili wa Sheria ujitegemee kabisa na Rais asiwe na amri kwayo.
-Mwanasheria Mkuu asiteuliwe na Rais, iwe ni ajira itakayo thibitishwa na Bunge.
-Vyeo vya Wakuu wa Mikoa viondolewe na kuwe na Magavana wa kuchaguliwa na wananchi.
-Wakuu wa Wilaya waondolewe kubaki na Mkurugenzi wa Maendeleo aliye ajiriwa na Halmashauri za Wilaya atawajibika kwa Baraza la Madiwani.
-Wakuu wa Idara wilayani waajiliwe na Halmashauri na wawajibike kwa Baraza la Madiwani.