Mrimi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 1,691
- 640
Nimekaa hapa leo nikawa najiuliza ni kipi bora kati ya kilimo na ufugaji..nikawa nafikiria kufuga n'gombe wa kienyeji ambao kimsingi wana soko kubwa hapa nchini..changamoto kubwa kwa haraka haraka ni uendeshaji;hasa eneo la kutosha la kufugia na malisho..lakini pia majira ya kiangazi kunakuwa na shida sana ya malisho na hasa ukizingatia kwamba hawa jamaa wanachelewa sana kukua..kuhusiana na magonjwa sikuona kama ni changamoto kubwa sana..
Kuhusiana na ng'ombe wa kisasa nikawa nafikiria je,nifuge wa nyama au maziwa? Nikajaribu kuangalia soko la maziwa lipo japo ktk eneo ninaloishi bei ya maziwa si nzuri..kwa hiyo nikaona kama output ni ndogo relatively to input..ng'ombe wa nyama wa kisasa soko lipo..ila changamoto ni namna ya kupata mbegu bora na eneo na gharama za chakula..
Nikageukia kilimo,hasa cha mazao ya chakula..changamoto kubwa ni bei ya soko na mabadiliko ya hali ya hewa..hapa eneo la kulima halikuwa changamoto sana na hata gharama za uzalishaji sikuona kama ni tatizo sana kwa kuanzia..
Wazo langu la ufugaji lilikuwa nianze kwa kununua ndama 20 kwa kuanzia halafu nikomae nao hadi baada ya miaka 3 nione nitakuwa nimepata nini..then kama mazingira yakiruhusu niongeze tena wengine..
Baada ya kutafakari sana nikajikuta kama nimeishafeli hata kabla ya kuanza! Ndipo nikaona nipite mitaa hii nipate uzoefu kwa wengine..na ktk hili nahitaji kufahamu kama nitawekeza kwa mfano tsh 20mil..ktk aidha kilimo au ufugaji ng'ombe,je baada ya hiyo miaka 3 ni wapi penye unafuu na maslahi zaidi?