Kipi bora, upate Mwenza 'mwingi' lakini anakujali, mnasikilizana, anakuheshimu au Mwenza Mtiifu lakini amezubaa, kisirani

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Wengine huita 'mood swing'

Kwa watu wazima wote nadhani tayari tuna uzoefu wa kuishi Wawili chini ya paa moja kwa muda, kama wenza, Mke na Mume, huku wote mmekutana mkiwa na historia tofauti za kimalezi.

Sasa je, kipi bora kati ya Watu wa aina hizo mbili. Yaani Mwenza wa kujichanganya sana na Marafiki, simu yake ipo bize muda mwingi...lakini akifika nyumbani anaamshaamsha, ana maneno mazuri, matamu...ukimwambia unajisikia vibaya ana "react" hapohapo...atampigia dokta au atakimbia duka la dawa...au kama ni kuandaa dawa asili(home remedy) ataingia jikoni hapo hapo bila kujiuliza mara mbili.

Au uwe na mwenza mtiifu wa ndoa, ambaye akitoka tu kazini breki ya kwanza nyumbani, lakini ndio hata akikukuta kitandani hakuulizi kulikoni...ukimwambia unaumwa akijitahidi sana atakuuliza "umeshaenda hospitali?" zaidi ya hapo atatulia tuli kwenye kochi asubiri msosi akalale.
 
Mzimu
 
Inategemea wewe ni mtu wa vp wapo waliozubaa na wamekutana wote wa kuzubaa na maisha yao yanaenda tu vzur
 
Ila hapa nimezilenga jinsia zote mbili.
 
Mwingi
NDO anafaa sana kikubwa nitajitahidi kununua kondom au kumpa ushauri kadiri iwezekanavyo kwenye mwingi mwingini wake
 
Mwingi
NDO anafaa sana kikubwa nitajitahidi kununua kondom au kumpa ushauri kadiri iwezekanavyo kwenye mwingi mwingini wake
Mmh, kuongea ni rahisi...kabisa ushtukie anakula pisi kali mahali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…