Kipi cha muhimu zaidi, kipi nakipenda zaidi, niko teari kuacha vingapi ili nipate kimoja

Kipi cha muhimu zaidi, kipi nakipenda zaidi, niko teari kuacha vingapi ili nipate kimoja

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
459
Reaction score
653
MARGINAL RATE OF SUBSTITUTION

Hii theory inaelezea tabia ya mwanadamu ambayo inaendana na ile concept ya choice making.

Hii concept itakusaidia kujua kitu gani unakipenda zaidi ya kingine japo vyote ni muhimu kwako na vyote vina kupa tulizo la nafsi.

Mfano 1:

Kama kwenye mchoro unavyoonyeshwa, hii ni perfect substitute kwamba kuna juice ya apple glass 1, na kuna juice ya chungwa glass 1.

Upo teari kuacha kipi ili upate kipi?

Mfano 2:

Umepewa likizo ya siku 1, wazazi wako wanaishi mikoa tofauti kwaio utapata nafasi ya kuchagua kati ya kwenda kumuona mama au baba.

- Wote ni wazazi na unawapenda sawa, ila hii theory inatusaidia kujua kipi ambacho kitakupa furaha zaidi ya kingine japo vyote ni sawa.

Kwaio kwenda kumuona mama au baba , utakachochagua hapo ndio tunakiita marginal rate of substitution

Mfano 3:

Umeletewa sahani moja ya biriani na sahani nyengine ina sambusa 10.

Huu mfano unaonyesha kwamba mda mwengine kula sahani moja ya biriani ni muhimu sana kwako kuliko sambusa 10, japo zote ungeshiba na unge enjoy kuzila maana unapenda vyote sawa.

Mfano 4:

Unatakiwa kuoa, ila una wachumba watatu na wote wana elimu sawa, uzuri sawa na vyengine vyote wanaendana.

Sasa kitendo cha wewe kuamua kumchumbia 1 nakuacha wengine inamaanisha kuwa yule 1 ni bora zaidi ya hao wawili uliowaacha.

Kwamaana nyengine ni kwamba yani wale wawili ni sawa na huyu 1 ambaye umeamua kumchumbia.

Mfano 5:

Ukifungua biashara yako utapata hela, pia ukiamua kuajiriwa utapata pesa. Tuna assume faida utakayopata kutoka kwenye biashara ni sawa na salary utakayolipwa ukifanya kazi.

Sasa kitendo cha wewe kuamua kuchagua kimoja na kuacha kingine hio ndio marginal rate of substitution.

Mfano 6:

Unahitaji kuolewa, kuna wanaume wawili, mmoja anahofu ya Mungu, mwengine ana pesa za kutosha. Wote wanakupenda sawa, wote wanakuthamini, wote wanavitu vyengine sawa. Kitendo cha wewe kuchagua mmoja na kumuacha mwengine inamaana uko teari kumsubstitute mwenye hofu ya Mungu ubaki na mwenye mali au vice versa.

Mfano 7:

Kipindi cha barter trade, mtu ana exchange mayai 20 kwa gunia 1 la mahindi, hii inaonyesha kuwa hivyo vitu vina same rate of marginal substitution.

Mfano 8:
Kuamua kutokuoa ili ukae nyumbani na kutunza wazazi au kuamua kuoa na kuanzisha familia mpya. Tunaona kuwa kote ni familia, wazazi ni muhimu ila pia kuwa na ndoa na kuwa na watoto ni muhimu.
Decision ya ku substitute kimoja na kuchukua kingine ndio marginal rate of substitution.

Main point ni kwamba sio lazima vitu vilingane kwa quantity, ila ile satisfaction unayoipata inakuwa inaendana. Vyote viakupa faida ila kimoja uko teari ukipate zaidi at cost of letting go the other thing.

Sawa na mtu akwambie niko radhi niache mali zangu zote ili niwe karibu na Mungu au Kitendo cha mtu kuamua kuacha kazi ili awe karibu na familia nk

#substitute #marginalrate #decisionmaking #marginalrateofsubstitution
marginal rate of substitution for perfect substitutes.png
image_thumb8.png
 
Back
Top Bottom