Kipi cha pekee na tofauti (special) kwa Wema kwenye bongo movie?

pathfinder_tz

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2018
Posts
356
Reaction score
377

Watanzania mnayapata wapi mapenzi ya Wema Sepetu kwenye bongo movie?

Kipi special kwa Wema ambacho anafaa kupewa tuzo ya Best actress?

Nimeangalia Heaven Sent ni movie ya kawaida sana ambaye Wema anajifanya mwema na mshamba mpaka pale anakutana na Gabo.

Watanzania tuache double standard, Wema kwenye movie ambayo imempa tuzo mbili ni very normal.

By the say kuna movie nimeiona kibongo bongo inaitwa Fatuma, its a hell of a movie Director na waigizaj wanajua sana pia setting ya movie na story very unique.

Tuliobahatika kuiona ile movie ya wakenya inaitwa Watatu ni movie nzuri sana na imestahili kujishindia tuzo zile ambazo imepata, movie imeandaliwa miezi sita na walivyoona tayari wakamleta mtu kutoka USA kuja kuidirect na kutoa ujuzi tofauti tofauti na ilivyokamilika, imestahili.

Sasa basi Wema kupewa best actress na viewers choice award ni vile tu anamashabiki wengi wa kumpigia kura na isitoshe watanzania wanapenda ushabiki badala ya kazi.

Hii ni changamoto kwenye tasnia ya filamu na sanaa kwa ujumla. Mtu apewe anachostahili kutokana na ubora wa kazi yake but isiwe kwa mapenzi tu kwa kufika hivyo tasnia itafika pale watu wanapotaka ifike like watapenda zaidi na watakosa maneno ya kukosoa.

Kina Lupita Nyong'o walipata platform na wakaitumia vizuri hakuna ku fake vitu, wanatumia kipaji na taaluma professionalism hakuna kubebana.

Tukumbuke we r miles away kuwa nominated kwenye Oscars na tuzo zngine mashuhuri kama tukiendelea kubebana na kushabikia watu badala ya kazi.

God bless Tanzania God bless bongo movies
 
"Kisa wo.wo.wo." Na wanaoangalia huo ulimbukeni wa Bongo movie, webgi wao, ni kina mama.
 
Jiandae kupingwa na wenye timu zao na wenye mahaba yao bila kuangalia uhalisia na ukweli wa mambo.
 
Ni kweli wema sii msanii mzuri ila kilicho m'beba kwenye hizo tuzo zao ni kura za mashabiki wake.
 
Ulitaka apewe nan tuzo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…