Kipi chanzo cha Ugomvi wa Shetani na Mwanadamu

Mkimuyangu

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2022
Posts
1,054
Reaction score
1,947
Napenda kukalibisha uchangiaji wa maada,ili watu wapate kujua,kutokana na ukubwa wa elimu za Dini tofauti

Sipendi michango ya matusi au kukashifu Dini ya mwingine,kwani naamini hakuna Dini au dhehebu linalofundisha waumini wake matusi
 
Tunda la mti wa katikati
Hivi inaingia akilini kweli?wakagombana tu sababu ya tunda la mti wa katikati,na hilo tunda linaitwaje,ni kati ya haya matunda tuliyonayo duniani? Mbona hamna tunda lililokatazwa tofauti na nguruwe na pombe?
 
Mungu alipomuumba Adam na Hawa aliwaambia wazae waongezeke waijaze dunia. Lakini aliwaambia mti wa katikati wasiule matunda yake (wasifanye mapenzi kinyume na maumbile)

Shetani akamfundisha Hawa ushetani. Hawa akamfundisha Adam.

Baada ya uchafu huo, Mungu akawapiga laana nyoka na Hawa na kuwafukuza Eden.

Baada ya hapo Mungu akaweka uadui mkali kati ya shetani a.k.a joka na uzao wake against Hawa na uzao wake
 
Napenda kukalibisha uchangiaji wa maada,ili watu wapate kujua,kutokana na ukubwa wa elimu za Dini tofauti

Sipendi michango ya matusi au kukashifu Dini ya mwingine,kwani naamini hakuna Dini au dhehebu linalofundisha waumini wake matusi
Mambo yote yalipangwa yakapangika yenyewe!

Hakuna coini kama tunavoaminishwa!!
Kama JINSI ilivopangwa wewe kuwa wa motoni au mbinguni peponi!

Coz

Yeremia anaambiwa *kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu nalikujua"kwahio yote yamepangwa hakuna suprise mkuu!!
 
Napenda kukalibisha uchangiaji wa maada,ili watu wapate kujua,kutokana na ukubwa wa elimu za Dini tofauti

Sipendi michango ya matusi au kukashifu Dini ya mwingine,kwani naamini hakuna Dini au dhehebu linalofundisha waumini wake matusi
Chanzo cha ugomvi kati ya Shetani na Mwanadamu?
 
Chanzo chake si pale ambako shetani alimuingia nyoka na kuwa danganya wakina adam na hawa kula lile tunda ambalo walikatazwa wasile
 
Mbegu ni neno, idha neno la Mungu au la shetani. Mbegu huzaa matunda. Mungu alimkataza Adam asile matunda ya mti wa katikati, yaani Adam asipokee mafundisho ya mashetani.
 
Mungu alipomuumba Adam na Hawa aliwaambia wazae waongezeke waijaze dunia. Lakini aliwaambia mti wa katikati wasiule matunda yake (wasifanye mapenzi kinyume na maumbile)

Shetani akamfundisha Hawa ushetani. Hawa akamfundisha Adam.

Baada ya uchafu huo, Mungu akawapiga laana nyoka na Hawa na kuwafukuza Eden.

Baada ya hapo Mungu akaweka uadui mkali kati ya shetani a.k.a joka na uzao wake against Hawa na uzao wake
Hii ndiyo nasikia leo,sijawahi kusikia toka nizaliwe,mbona hakuna kitu katika vitabu vya mungu kinachofichwaga,sasa kwa nini walitumia lugha tata
 
Mbegu ni neno, idha neno la Mungu au la shetani. Mbegu huzaa matunda. Mungu alimkataza Adam asile matunda ya mti wa katikati, yaani Adam asipokee mafundisho ya mashetani.
Endelea kufafanua naona kama umeishia njiani?
 
UZURI WA BIBLIA HAIFICHI KITU.

MWANZO 3.13-16.
Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
Mwanzo 3:13

14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Mwanzo 3:14

15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Mwanzo 3:15

16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Mwanzo 3:16

AGANO JIPYA KITABU CHA UFUNUO.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Ufunuo wa Yohana 12:9

17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu;
Ufunuo wa Yohana 12:17
 
Inawezekana Biblia ikawa ilieleza kila kitu?au ingeeliza kila kitu kitabu kingekuwa kikubwa tungeshindwa kubeba

Haya ni mahojiano ya Msigwa ya Leo.

Screenshot_20230506-150543.jpg
 
chanzo kikuu cha ugomvi kati ya binadamu na shetani ni WIVU.

Shetani ana wivu mkubwa sana. kabla ya kuumwa kwa binadamu Mungu alitoa ufafanuzi kidogo jinsi binadamu atakavyokuwa kiumbe cha kipekee na chenye uwezo mwingi hata wa kuwaongoza malaika na viumbe vingine. Shetani hapo hakuelewa somo, akaonesha wivu mkubwa na miswali kbao kwa Mungu kwanini mwanadamu awe hivi? kwanini vile?

kumbuka kabla ya kuumbwa kwa binadamu shetani kama malaika alikuwa na mauwezo mengi plus maujanja na uongozi wa juu. lakini Mungu alisema binadamu ndio atakuwa top.
 
UZURI WA BIBLIA HAIFICHI KITU.

MWANZO 3.13-16.
Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
Mwanzo 3:13

14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako;
Mwanzo 3:14

15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Mwanzo 3:15

16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Mwanzo 3:16

AGANO JIPYA KITABU CHA UFUNUO.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Ufunuo wa Yohana 12:9

17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu;
Ufunuo wa Yohana 12:17

Kaka hapo kwenye nyoka kulaaniw hapo mhhh mi hapana coz hatukuwahi kusikia nyoka atembelee miguu kabla nyoka ni mwendo wa tumbo tu

Kwani kabla ya laana nyoka alikuwa anatembelea nini?! Mpaka alalaaniwa atembelee tumbo
 
Back
Top Bottom