Kipi chuo kikuu bora Tanzania?

tommyy

Senior Member
Joined
Mar 7, 2013
Posts
178
Reaction score
85
Mm ni muhtimu wa kidato cha 6 natarajia kujiunga na chuo kikuu mwaka huu ni kipi chuo bora wakubwa,nielekezeni mdogo wenu na munipe sababu kw nn ni bora?
 
Kama wewe ni kipanga nenda pale mlimani, lakini pale wanataka vichwa!!!!Kama ulipata marks za kuhesabia mfukoni, usijaribu hata kufanya application!!!

Tiba
 
Cku hizi watu hawaangalii vyuo vizuri wanaangalia kozi nzuri, unataka kusomea nini? Ila chuo kikuu udsm kizuri ila kigumu sanaa
 
tommyy, vyuo Tanzania hii ni vingi, Je unaongelea uboea wa chuo katika nyanja ipi? Michezo, Majengo, Mazingira au?
Kama ni elimu unaongelea chuo katika kozi (z)ipi?

Swali zuri sana. Hivi ubora wa chuo unapimwaje? Ubora wa elimu? ufanisi wa utendaji wa graduates? Majengo? Maprofesa wazuri?
Chuo kinachotoa effective graduates hicho ndo chuo bora kwangu.
 
Last edited by a moderator:
Mzumbe na SUA wazuri pia! Wana waalimu wazuri/wazoefu... hakuna mogogoro mwanafunzi anamaliza kwa muda uliopangwa!

Pia idadi ya wanafunzi sii kubwa kama UDSM hivyo ni rahisi mwalimu kufuatilia maendeleo ya mwanfunzi!
 
Subiri matokeo dogo... Umeona wenzio wa form four walivyonyolewa?! Sasa na wewe tulia tuli usubiri matokeo, ukifaulu vizuri njoo na hoja yako.
 
amazon college! au magomeni secretarial college!
 
Kama wewe ni kipanga nenda pale mlimani, lakini pale wanataka vichwa!!!!Kama ulipata marks za kuhesabia mfukoni, usijaribu hata kufanya application!!!

Tiba
Haswaaaaa. TZ Nzima hakuna Kama UDSM mpaka sasa
 
subiri matokeo usijekua umezungusha university kinapatikana mtaa wa Necta
 
Je matokeo yako na wewe ni mazuri? Subiri Ndalichako atangaze kwanza. Ila mwaka huu mtafaulu ili ile soo ya form IV isirudi kabla Tz hatujasahau
 
udsm baba yao, kinafwata SUA, Mzumbe,Muhimbili....vingine ni vyoo vikuu...nasapoti kauli ya Dr Lymo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…