Kipi kilibinafsishwa kikawa na ufanisi na tija Tanzania?

Kipi kilibinafsishwa kikawa na ufanisi na tija Tanzania?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Kuna watu wanasema Watanzania wameshindwa kujisimamia, naomba watueleze ni eneo gani kampuni za Kigeni zimewahi kupewa Tanzania ikanufaika.

Tumekuwa wepesi Sana kuvuruga wananchi na watendaji Kwa malengo ya kisiasa tunapotaka kuuza rasilimali. Tumewekeza fedha nyingi Sana bandarini ,tukawekeza fedha nyingi kwenye ulinzi wa Mali halisi then tunakabidhi wageni. Kwani Watanzania wakiiba inatuuma nini Hadi tuone wageni ndio wanapaswa kuiba.

Tumeona Kitenge na timu yake wakipelekwa Uarabuni kwenda kurekodi kipindi, tuliona Loliondo alifanya ze same, tuambieni mnapowafanyia haya wananchi mnapata faida gani.

Tumewadharau Watanzania Kwa muda mrefu na kuwapa value wageni tukiamini Sisi tupo hapa Daima Ila tutakufa tu. Jiulizeni wapi mmewahi kubinafsisha na Sasa makusanyo ya Kodi yameongezeka.

Bandari inakusanya trilion 7 Kwa mwaka, then Sisi tunawaza kufikia trilioni 27 baada ya miaka 30 na tunaona huu ni ufanisi; tujiulize value ya trilioni 30 miaka 30 mbele inatofauto na uzalishaji wa trilion Saba wa Leo.

Tunapokaa nakutafakari maendeleo tusidharau population ya watu milioni sitini tukaamini familia zetu Ndizo Tu zina 1atu sahihi. watoto wa viongozi wamejazana bandarini si Kwa ufanisi Bali wamepewa ulaji then tunahoji ufanisi; how
 
Kuna watu wanasema Watanzania wameshindwa kujisimamia, naomba watueleze NI eneo gani kampuni za Kigeni zimewahi kupewa Tanzania ikanufaika;
Na hili litapita tu, watanzania tulisha wazoea ni waoga na chawa.
 
Umeruka tatizo halisi, mkuu. Hoja si ubinafsishaji ama utaifishaji. Hoja kuu ni uzalendo na maadili ya watumishi, kuanzia yule bosi wao.
 
Back
Top Bottom