Kipi kimesababisha ongezeko la mauaji kwa wanandoa na wapenzi

Kipi kimesababisha ongezeko la mauaji kwa wanandoa na wapenzi

Utawala2025

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2023
Posts
1,144
Reaction score
2,755
Habari.

Karibuni kwa kujadili hii mada natumaini ninaweza kupata uzoefu(Experience) zaidi kuhusiana masuala ya ndoa na mahusiano.

Kumekuwa na wimbi kubwa la ndoa nyingi kuvunjika,migogoro ya muda mrefu na inayopelekea kuongezeka kwa mauaji gains ya wana ndoa au wapenzi na hali kujiua wenyewe au kujinyonga.

Je ni kipi kinapelekea ongezeko la wanandoa au wapenzi kujiua au kuuana na kipi kifanyike katika jamii ili kupunguza hali hii?
 
Usaliti hasa wanawake wamekuwa na tamaa sana na wanawake wengi wakisaliti dharau ndani ya nyumba inakuwa kubwa sana, ila kama ni mjanja ukishaona mkeo kazidisha dharau jua tu ana kidume nje ili kukwepesha mambo kama yakuja kuuana ondoka kimya kimya tu pamoja ni ngumu sana!
 
Vijana wengi wanaopenda kutumia hisia badala ya akili kujihusisha kwenye ndoa ,na vijana wengi wajanja na wenye kupenda kutumia akili kuzikataa ndoa.
 
Usaliti hasa wanawake wamekuwa na tamaa sana na wanawake wengi wakisaliti dharau ndani ya nyumba inakuwa kubwa sana, ila kama ni mjanja ukishaona mkeo kazidisha dharau jua tu ana kidume nje ili kukwepesha mambo kama yakuja kuuana ondoka kimya kimya tu pamoja ni ngumu sana!
Pole sana mkuu
 
Usaliti hasa wanawake wamekuwa n
a tamaa sana na wanawake wengi wakisaliti dharau ndani ya nyumba inakuwa kubwa sana, ila kama ni mjanja ukishaona mkeo kazidisha dharau jua tu ana kidume nje ili kukwepesha mambo kama yakuja kuuana ondoka kimya kimya tu pamoja ni ngumu sana!
usaliti tu

Ile ni sexual jealousy hasa wanakuaga nazo wanaume mana kama ni usaliti wa ndoa hata wao wanafanya. Wanaume tunachepuka San tu ila akichepuka mke inakaa fundo kwenye shingo mwaka mzima yani shari tu
 
Tatizo tunakosea mwanzoni kabisa,kama mahusiano yenu haya kujengwa kwenye misingi ya upendo, halafu mmoja akawa mwaminifu/anajitoa sana kuliko mwengine haya lazima yatokee. Kwani upendo huvumilia,husamehe na husahau.

Siku hizi mwanaume ataangalia uzuri,hata kama huyu mwanamke hampendi,mwanamke ataangalia hela hata kama mwanaume huyo hampendi na hajamvutia/anamnyanyasa ndio maana siku hizi kuna kauli mbiu ya mabinti/wanawake bora kulia kwenye V8 kuliko kucheka kwenye guta au kuna msemo wao mpya wanasemaga bora vita kwenye wali nyama.

Bila kusahau zile gender role zishaharibiwa kwa usasa na maswala ya haki sawa ,so lazima tu cheche ziwake, hapo ndipo michepuko inapopata nafasi na kusalitiana huanzia hapo.
 
Kupenda kupitiliza na wanawake wengi sikuhizi wamevurugwa
 
Tatizo la kung'ang'ana kwenye mahusiano. Tujifunze kuwaacha waende kwa amani. Kuwa na matarajio makubwa kwa wenza wetu. Kutojifunza kuishi bila wao, ishi maisha yako, usitegemee mtu kukamilisha maisha yako.
 
Back
Top Bottom