Tatizo tunakosea mwanzoni kabisa,kama mahusiano yenu haya kujengwa kwenye misingi ya upendo, halafu mmoja akawa mwaminifu/anajitoa sana kuliko mwengine haya lazima yatokee. Kwani upendo huvumilia,husamehe na husahau.
Siku hizi mwanaume ataangalia uzuri,hata kama huyu mwanamke hampendi,mwanamke ataangalia hela hata kama mwanaume huyo hampendi na hajamvutia/anamnyanyasa ndio maana siku hizi kuna kauli mbiu ya mabinti/wanawake bora kulia kwenye V8 kuliko kucheka kwenye guta au kuna msemo wao mpya wanasemaga bora vita kwenye wali nyama.
Bila kusahau zile gender role zishaharibiwa kwa usasa na maswala ya haki sawa ,so lazima tu cheche ziwake, hapo ndipo michepuko inapopata nafasi na kusalitiana huanzia hapo.