Kipi kinapelekea kuamua kufuta comment yako kabla haujaipost?

1. Nikiwa sipo sure au sikijui kiundani kitu nachotaka kuandika, NAFUTA

2. Nikihisi kitamkwaza mtu pasipo umuhimu, NAFUTA

3. Nikiona ni member ambaye itikadi kali, huwa NAIGNORE kabisa maana peace of mind muhimu
 
Sababu zako ni kama zangu.
 
Muda mwingine kunakuwa na maneno makali unayaandika bila kufikiria kutokana na hasira, baadae ukiangalia ulichoandika unajishangaa inabidi ufute tu.

Pia kitu Kama sina uhakika nacho huwa nafutilia mbali,

Au naandika kitu alafu nafikiria, "hivi lazima Nicomment? Kwanini Nicomment?, Alafu nafutilia mbali.

Mimi muda wowote naweza kubadilika, hata Sasa hivi naweza nikaifuta, mimi wa sasa hivi na mimi wa dk5 zilizopita ni watu wawili tofauti.

Hivi ulisema kabla ya kupost vile!!?..
 
Nakijua kichwa changu kinavyotapika pumba..Kila nikichangia kitu after 24hrs lazima nirudi kufuta comments zangu. Landa uwe uzi nilioanzisha mm.

Kuna wakati nasoma comments zangu hadi najionea aibu.. (hata hii comment itafutwa)
Hii ipo gud boss.
 
Pamoja mkuu.
 
Mimi kuna mada nyingi sana, hasa zile ambazo zimegubikwa na uongo mwingi, au tuhuma.

Mfano wa mada hizi huwa napita tu kimya kimya, na ikitokea nikaandika basi aidha nafuta au naandika "Nimesoma maoni yote" au"Naendelea kusoma maoni ya wadau".
Pamoja Chief.
 
Kuna muda unakuta mada unaamua kuchangia. Unaanza kuandika kisha unaona ni mizenguo tuu unaamua kufuta ulichoandika kabla haujapost.
Ni sababu ipi inapelekea unaifuta comment yako badala ya kuipost?
reflection.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…