Kipi Kiswahili fasaha, kwa majina au kwa jina?

KIDO123

Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
18
Reaction score
29
Wadau kuna maneno yanatatiza ,
Ukifuatilia vyombo vya habari siku hizi kwenye mahojiano, au popote pale kwenye maisha ya kila siku, pindi mtu anapopewa fursa ajitambulishe utasikia anaanza kusema kwamajina naitwa fulani bin fulani,
Swali langu kwa wajuvi ipi sahihi kati ya KWAMAJINA AU KWAJINA
Halafu hii kwamajina wanatumia sana wakenya naona sasa imeingia tanzania
 
Wote wapo sawa..ukiulizwa Jina lako nani Utajibu Mansosa ila ukiambiwa taja majina yako Utajibu Mamsosa Tupilike Andendekisye.
 
Kwa majina siyo sahihi kwa sababu ni wewe ndiyo unajitambulisha kwahiyo hata ukitaja jina la baba,babu hilo lote ni jina lako,kwahiyo unasema jina langu fulani... basi.
Wengine utasikia wakisema "Naitwa fulani" Uitwi na mtu yeyote wewe sema tu jina langu fulani...... basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…