Jina kazi yake ni kumtambulisha mtu na mara kadhaa kwa kumtofautisha au kumhusisha na watu wengine(wakati mwingine vitu) ambao tayari wanajulikana.
Inategemea pia ni nani anaita:
- Kama ni mtoto wake (ataita "mama")
- Kama ni mume au watu wengine wanaofahamu kuwa ana mtoto anaitwa mafaume (wataita "Mama Mfaume")
- Watu wanaofahamu kuwa ameolewa na Mumewe anaitwa Kikwete na pengine hawajui kama ana mtoto au hawafamu majina ya mmojawapo wa watoto wake (wataita " Mama Kikwete" - Mama hapa inabadilika maana na kuwa 'mke wa' au 'Mrs')
Mazingira pia yanaweza kubadili jinsi ya kuita: kwa mfano mama yako akiwa kwenye umati wa kina mama, utamwitaje?
Kumbuka kuwa kimazoea, si 'adabu' kumuita mama mtu mzima (aliyekuzidi umri) kwa jina lake la mwanzo katika mazungumzo au mawasiliano ya kawaida ya kinyumbani na yasiyo rasmi (informal). Wazungu wenzetu hii siyo shida kabisa!