Black BackUp
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 717
- 666
Habari zenu wadau,
Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.
Hivi hapa Jijini Dar es salaam nini haswa chanzo cha foleni katika barabara zetu kati ya taa za barabarani au traffic?
Je, trafiki ni chanzo, maana wanasimama mpaka kwenye roundabout, barabara za mitaani pamoja na kwenye maeneo mengine.
Hivi kwani vipi wakiachia taa zifanye kazi yake maana taa zimedizainiwa kuruhusu magari kwa muda maalum kila upande bila kuongeza ama kupunguza muda.
Toa maoni yako maana yako
Huku niliko taa zenyewe wameziseti kikuda kuda tu,Red inawaka kwa sekunde 120(dakika 2) afu Green inawaka kwa sekunde 30(nusu dakika),kama si kulostishana huko.
Kweli kabisa asilimia kubwa hawa jamaa (traffic) kama hawapo barabaran foleni hua hakuna ama folen hua inatembea... Wakikaa tu balaah linaanzaMandela road kukiwa na traffic foleni inakuwepo,wakiondoka au wakiwa wamechelewa kufika foleni hakuna. Mataa yanafanya kazi nzuri kuliko askari ambao hawaeleweki
Huku niliko taa zenyewe wameziseti kikuda kuda tu,Red inawaka kwa sekunde 120(dakika 2) afu Green inawaka kwa sekunde 30(nusu dakika),kama si kulostishana huko.
Hiyo ni ya pale Africana nini, maana km unatokea Salasala magari yanayoweza kupita hayazidi 4 then Red light inawaka,lbd wave wamerekebisha !