Wakuu,
Natumaini wote tumesikia kuwa Serikali itatumia jumla ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya Vitambulisho. Haya yanafanyika wakati karibu watoto milioni 4 wa shule zetu za msingi wanakaa chini na mbaya zaidi hali ya vitabu katika shule zetu zote ni ya kukatisha tamaa. Sekondari za kata ndiyo usiseme. Binafsi sioni umuhimu wa kutumia shilingi bilioni 200 kwa ajili ya vitambulisho wakati elimu yetu iko ICU.
...Na hili ndilo jibu la "Kwa nini nchi yetu ni masikini sana baada ya miaka yote hiyo ya uhuru". Hatujui tuanze na nini cha muhimu na tumalizie na kipi kingine! Watu hawana makazi kilosa kutokana na mafuriko, wanahitaji makazi bora, lakini sie twakimbilia kuchapa vitambulisho...Serikali yetu haina vipaumbele.
Ndugu yangu vyote ni muhimu labda ungesema kipi kipewe kipaumbele..lakini ukumbuke kwamba changamotoya vitabu na madawati ni tatizo sugu hapa nchini hivyo hata kama vitambulisho vikiwekwa pembeni bado pesa hizi zitaelekezwa kingine..tatizo ni priorities.
Wakuu,
Natumaini wote tumesikia kuwa Serikali itatumia jumla ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya Vitambulisho. Haya yanafanyika wakati karibu watoto milioni 4 wa shule zetu za msingi wanakaa chini na mbaya zaidi hali ya vitabu katika shule zetu zote ni ya kukatisha tamaa. Sekondari za kata ndiyo usiseme. Binafsi sioni umuhimu wa kutumia shilingi bilioni 200 kwa ajili ya vitambulisho wakati elimu yetu iko ICU.
watakuja na sarakasi nyingi sana, personally sijaona hivyo vitambulisho vya uraia kwa nchi yetu vitasaidia nini, yaani watu wanajifanya kama sisi ni USA,! kuna interaction kubwa mipakani.
Bado kama tumeshaprove ufisadi, hivyo vitapatikana tu hata ambaye si raia, tena wanavyotangaza wengi watakuja watavichukua na kurudi makwao
Tulishapoteza system za ubalozi wanyumba kumi kumi, kutoa taarifa kwa mtu mgeni anayepanga mahali, vyeti vya kuzaliwa n.k
kwa mfano tungesema lazima kila raia awe na cheti cha kuzaliwa, na mtu anaanza kukitumia kuanzia anapoingia darasa la kwanza na kuwenye huduma nyingine muhimu za jamii!
Hii haina tofauti na alichosema JK 'flyovers' yaani tunawaza mambo makubwa bila kuprove au kuonyesha haya madogo yameshindikana
Kinachonifurahisha hoja hii ya vitambulisho bungeni wote wanaitetea kua ni muhimu!! For now our system is corrupt na hakuna ground zozote zilizowekwa kuzuia huu ufisadi! Bilioni 200 zitatumika then what? kila mtu hata asie raia atapata hicho kitambulisho!! ila Elimu itabaki vile vile na hao ambao sio raia wenye ID yetu ndo watachukua kazi za watoto wetu!! Nimesikitishwa na Taaarifa kua Form 4 exam Zero 65,000!! wataenda wapi hawa?