Kipigo cha Al Ahly kwa Simba ni fedheha kwa wachambuzi maandazi waliojazana hapa nchini

Kipigo cha Al Ahly kwa Simba ni fedheha kwa wachambuzi maandazi waliojazana hapa nchini

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Ilikuwa ni kero kuwasikiliza mara nyingi wakikumbushia goli 5 wao wakiziita hamsa. Hakuna aliyejali ushindi wa Simba na pointi 3.

Sasa leo najua itakuwa fedheha sana kwao kwani hawatakuwa na lolote against Simba. Ila nijuacho ni suala la muda wa siku tatu tu wataanza kukumbushia mechi ya marudiano. Hawajui kuwa Simba ana point 6 na anaongoza kwenye kundi. Wao wana ushabiki wa ndondo wa kufungana tu bila malengo.

Ushindi wa Simba na utaleta fadhaa sana kwa wachambuzi utopolo waliojaa kwenye vyombo vya habari.
 
Nchi nyingine wachambuzi ni wachezaji wastaafu/malejendi na wana badge za fifa kwenye ukocha ndio maana wanachokitabiri mara nyingi huwa kinafanana na matokeo baada ya mechi.

Hawa wa kwetu hawajaenda shule yoyote ya mpira ndio maana utabiri wao huwa ni negative na matokeo halisi. Mechi za nje Huwa wanakwenda kusoma uchambuzi wa kina paul shcoles, neville, rio, lampard, callager, bwalya, v boaz, giggs, owen, mourinho, evra na wengine wengi halafu wanakuja kutafsiri na kubwabwaja kwenye show zao na matokeo hayapishani kwa mechi za nje, sasa hizi mechi za caf hazina uchambuzi wa masoccer guru wa nje kwahiyo inawabidi hawa wabongo watabiri wenyewe na ndio hapa upumbavu wao unapojianika
 
Vineka kama hao tunajua namna ya kuishi nao..!

Hawazui chochote Simba SC inasonga mbele tu
Ahli ni lazima afe na vita mechi ijayo, na sisi tufe na msudani mechi ijayo cause tumepata confidence kubwa sana hii leo yaani tumpige vita kwake na ahli halafu tushindwe kumchapa msudani.. wasudani wenyewe wameshakubali kupoteza kisaikolojia kabla ya mechi.. huwenda tukawa timu ya kwanza kufuzu robo fainali, naamini point 9 zinatupeleka
 
Back
Top Bottom