Kipigo cha Al Ahly kwa Simba ni fedheha kwa wachambuzi maandazi waliojazana hapa nchini

Yaani misri hapakaliki mpaka muda huu yaani hawaelewi Mnyama kamtunguaje mmisri tena kwa kutandaziwa soka sambusa yaani unafungwa halafu na bado ukafurahia mtanange maana wao walikuja na matokeo yao mfukoni. Hawakujua mnyama atamkandamiza tena kwa mkapa sijui anasahau nini sasa wakati mwarabu pale kwa mkapa kichapo nicha kawaida tu na wala asiteseke saaana. Kuna mchezaji mstaafu wa misri alisema simba ndio ingekuwa ndo inaiogopa Aly ahly nilimzoom tu halafu nikamwambia atulize wenge. Pamoja na ubora wao lakini wamekaa tu.
 
Waarabu wana kaubaguzi flani ivi,ambao kama timu za mataifa ya weusi hasa West na Kusini mwa jangwa la Sahara wakizinduka na wao wakaanza kampeni za kuwabagua,waarabu watalalama sana.
 

Mkuu kibaravumba kuna uwezekano kwa taarifa (takwimu) walizokuwa nazo walikuwa sahihi kwavile mambo mengi (Technical Strategies) ya Simba kwa sasa watu wengi hawayafahamu. Ukiangalia simba kwa sasa wanakuja uwanjani na mkakati kulingana uwezo wa mpinzani wao (One Match at a time), yule wanayemwita "Match Analyst" waliyemwajiri toka SA anafanya mambo mengi (Havumi lakini yumo) ya kuzifanyia ukipenda "SWOT" timu pinzani kabla ya Match husika THEN Kocha anaandaa mpangokazi wa huo uchambuzi. Mambo haya ni gharama kidogo LAKINI ukitaka ufanikiwe kwenye football LAZIMA uwekeze Resource za kutosha.

Nimeandika kiuchambuzi kwavile mimi sio MNAZI hivyo niko tayari kusahihishwa.

Ahsante
 
upo sawqa ndugu kinachoboa ni pale mchambuzi anapojitafsiri kabisa kua yeye ni mnazi wa utopolo unadhani kuna zuri gani ataongelea kuhusu simba
 
Ishi maisha yako,waandishi wa habari hasa TZ hawajui wanachoandika .Utakubaliana na mimi angalia magazeti yetu ya michezo kila siku utashangaa
 
Hawa wachambuzi feki wanajaribu kubalance ushindi wa simba na upotolo alipobahatisha mara moja wanasahau timu inayoshiriki ni Simba na ipo kwenye klabu 20 bora za Afrika ingawa tunapoelekea kuna uwezekano itakuwa kwenye timu 10 bora Africa wanailinganisha na katimu ambako hakapo hata kwenye klabu 50 bora Africa
 
upo sawqa ndugu kinachoboa ni pale mchambuzi anapojitafsiri kabisa kua yeye ni mnazi wa utopolo unadhani kuna zuri gani ataongelea kuhusu simba
Sasa hivi wanasubiri onyango afanye kosa waanze kumponda
 
Uchambuzi sio utabiri. Wanaangalia hali halisi kabla ya mechi na kutoa mwelekeo wenye uwezekano mkubwa given the facts. Si lazima itokee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…