mapesa yamejaa
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 1,412
- 3,419
Mzee mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Manase amepokea kipigo kutoka kundi la vijana wamachinga hapa mjini Sumbawanga. Nikiwa nimetulia zangu hapa kwenye biashara zangu za madafu, mita kama 100 mbele yangu nikaona kundi linamkimbiza huyo mzee aliyevalia nguo za CCM huku akipigwa mawe na fimbo na wengine wanamrushia chupa za soda. Huruma ilinijia ikabidi niende kuamua huo ugomvi.
Cha kushangaza sababu niliyoambiwa ya kumpiga huyo mzee Manase ni kusifia awamu ya sita. Ana tabia ya kuwa akifika kwa wa machinga anaanza kuwaambia mama anaupiga mwingi mara oooh sasa hivi Nchi inalamba asali then anamalizia kwa kuwauliza au ninyi mnasenaje? Sasa vijana wanasema wamekuwa wakikereka sana na tabia yake huyo mzee.
Mimi nimeshangwazwa sana na tukio hili.yaani ndo tumefika huku kweli?. Pole sana Mzee Manase naamini unaendelea vizuri huko hosipitali.
Wasifiaji mjitathimini.