Dah! Inanikumbusha mbali sana... miaka kadhaa iliyopata wala dalili JPM atakuwa Rais.
Kuna timu moja kubwa sana tena hapa nchini ambayo imechukua ubingwa mara nyingi kuliko timu yoyote ile Tanzania hii.
Hii timu bhana, ambayo inaitwa Yanga ilikuwa na Mwenyekiti wake mmoja mtu wa hovyo sana. Basi bhana; watu wakasema kama mbwai mbwai tu kilichobaki ni kumuhujumu huyu Mwenyekiti!
Watu wakapiga hesabu Mwenyekiti ahujumiwe vp ili achukiwe na kila mtu?! Ikaonekana njia muafaka ni kwa hii timu kubwa ni kuiachia mabao mengi iwezekanavyo timu moja ya Mtaa wa Msimbazi!
Watu waliamini kwamba kv timu ya Msimbazi ilikuwa ni timu mbovu na dhaifu kupita maelezo; wanachama wa Yanga wangekasirika sana kufungwa na timu mbovu kama hiyo na hivyo wangemtimua Mwenyekiti kwa kuruhusu timu bora kufungwa goli nyingi na timu dhaifu!
Mpango ukasukwa barabara na ukasukikwa! Siku ilipofika; Yanga kwa makusudi ikajifanyisha na kuruhusu tugoli tutano kuingia kwenye nyavu na baada ya hapo uenyekit wa Mwenyekiti Llyod Mchunga ukaishia hapo!
Yaani ilikuwa ni Sting Operations mithili ya zile zinazofanywa na FBI au CIA!!
Dah! Yaani kuna timu zingine bhana... ndo maana haikushangaza baada ya ile Sting Operations Yanga wakaanza kujimilikisha makombe kila mwaka!
Sema tu walikosa ustaarabu manake wakasahau kabisa kuikumbuka ile timu ya Msimbazi ambayo ilisaidia sana kufanikisha Operation Timua Mchunga!
UJUMBE KWA YANGA: Akufaae kwa dhiki ndiyo rafikiyo...
Au, Usitupe jongoo na mti wake!