Kipimo cha presha ya damu

Kipimo cha presha ya damu

OCC Doctors

Senior Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
113
Reaction score
172
Shinikizo la kawaida la damu kwa watu wazima ni 120 kwa 80. Kipimo cha presha hupimwa kwa milimita za zebaki (mercury) (mmHg). Hivyo husomeka kama 120/80 mmHg. Shinikizo la damu hupimwa kwa milimita za zebaki (mmHg) kwa sababu kifaa kinachotumiwa kuipima, kinachoitwa 'mercury sphygmomanometer', kinategemea safu ya zebaki (mercury column) kuashiria shinikizo, kwasababu shinikizo la zebaki linakabiliana na shinikizo la damu.

Shinikizo au pigo la kusambaza damu kwenye mwilini huitwa (systolic) ambapo pigo la kawaida la kusambaza damu ni 120 mmHg. Hivyo (Systolic) ni uwezo wa moyo kusukuma damu kusambaa katika mwili. Uwezo wa moyo kujaza damu huitwa (diastolic) ambapo kawaida ujazo wake unatakiwa kuwa 80 mmHg. Hivyo shinikizo la damu ni uwezo wa moyo kusukuma damu na kujaza damu ambapo ni 120/80mmHg.

Word-Post.jpg
 
Back
Top Bottom