cupvich
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 408
- 247
Kamusi ya kiswahili ina eleza neno "Utajiri" kama neno la kiarabu likimaanisha wingi wa vitu vya thamani na wa vyanzo vya mapato ambayo nchi au mtu anamiliki. Katika karne hii ya 21 ambayo tunaishi, Tafsiri hiyo ya neno utajiri imechukua nafasi kubwa kwa kutuaminisha kuwa tajiri ni mtu yule mwenye mali nyingi au vyanzo vingi vya mapato kama vile Nyumba ya kifahari, Gari la bei kubwa, kiasi kikubwa cha pesa na n.k. Kipimo hichi cha utajiri wa mtu kwa kuangalia Mali alizonazo kwa kiasi kikubwa ni kipimo kinacho tazama muonekano wa nje zaidi (external context).
Kama ambavyo utajiri humaanisha wingi wa vitu vya thamani, wazazi wamekuwa na thamani kubwa katika maisha ya binadamu. Wazazi ndio wanaomwezesha mtu kuingia na kuishi katika dunia hii na baada ya kuzaliwa kumlea mtoto kwa uangalifu mkubwa na wema, wakimpatia mtoto chochote wanachoweza. Kwa ujumla thamani ya wazazi inazidi thamani ya vitu vyote ambavyo kwa pamoja vinafanya mtu awe tajiri.
Ni kwa namna gani Tunatumia nafasi zetu katika kuwatunza na kuwahudumia wazazi wetu?, je tumechukua nafasi yetu katika kuwajali kifedha, kisaikolojia au kiroho wazazi wetu? Kama ambavyo watu husema "mzazi ni mzazi hata kama ana upungufu wa akili". Nafasi yake inakuja kwasababu Alikuleta duniani na kuliona jua kwa mara ya kwanza. Hawa hawa wazazi wetu ndio wanaopitia changamoto mbalimbali katika makuzi ya mtoto hadi kuhakikisha mtoto anafikia malengo yake katika maisha.
Wakati mwingine wazazi wamepata watoto katika mazingira magumu na yanayotoa machozi na kuacha alama za maumivu katika maisha yao, wengine wamefikia hatua ya kutokwa na machozi pale tunapowakosea au kuwasahau. Wapo wazazi wanaolala njaa, walio na maumivu makali kutokana na maradhi lakini wengine wamefikia hatua ya kuvaa nguo moja mwaka mzima ilihali watoto wao wapo mijini pasipo kuwakumbuka na kuwatembelea ama kuzungumza nao kwanamna yoyote ile.
Tunaishi katika kipindi ambacho, wazazi wamegeuka Usumbufu na kero kwa watoto wao. Kiasi cha mtoto kujisikia vibaya anapopigiwa simu na mzazi wake wakati akiwa katika Kazi zake za kila siku. Vijana wengi wamekimbilia mijini kutafuta maisha na kuwaacha wazazi wao wakiwa katika hali mbaya vijijini kiasi cha mzazi kukata tamaa ya maisha. Hali hii imepelekea wazazi wengi kugeukia katika unywaji wa pombe ilimradi tu kujisahaulisha na machungu wanayopitia wanapokumbuka maumivu na mateso waliyopata wakati wakuzaa, kulea na kutunza watoto wao ambao wamewasaliti.
Thamani ya utajiri wa mwanadamu katika karne hii ya ishirini na moja(21) imeegemea zaidi katika vitu vya starehe na Anasa na kusahau jukumu kubwa la kuwatunza wazazi . Ni kawaida kwa mtu kumiliki kila aina ya kitu cha thamani mjini lakini wazazi wakiwa katika hali duni sana vijijini. Imekuwa ni kawaida ya wazazi kuwakumbuka watoto wao waliopo mijini kwa kuwapigia simu na kuwajulia hali kwani wanaona hiyo ndiyo fahari yao. Mzazi yupo radhi afunge mahindi na viazi kutoka kijijini na kumpelekea mtoto wake mjini. Kwa ujumla huu ndio upendo ambao tunapaswa pia kuwaonesha wazazi wetu. Imekuwa si ajabu kwa baadhi ya wafanyakazi kutumia likizo zao mijini kufurahi maisha bila ya kutenga walau hata wiki moja kwenda kuwasalimia wazazi kijijini. Hii imesababisha watoto kupoteza kabisa upendo kwa wazazi wao. Upendo ambao ulikuwepo tokea enzi za MABABU NA MABIBI zetu.
Qur'an tukufu katika sehemu ya aya ya 38 ya sura al Baqarah inasema ".....Hamtamuabudu yeyote ila mwenyezi Mungu na muwafanyie wema wazazi......." lakini pia Biblia takatifu katika kitabu cha Waefeso 6: 2-3 inasema " waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, upate heri,ukae siku nyingi katika dunia". Mwandishi Jalaja Bonhein(phd) katika kitabu chake kiitwacho KIFO NA KUFA, KUWATUNZA WAZAZI WETU WAZEE anasema " ...katika spishi zetu wenyewe, kuwatunza wazee ni sehemu muhimu ya kile inamaanisha kuwa binadamu. Kwa maneno mengine, mabadiliko ya jukumu tunayoweza kupata wakati wazazi wetu wanazeeka sio mbaya au bahati mbaya. Inatarajiwa.
Maisha wanayo ishi wazazi wetu ndicho kipimo sahihi cha kufanikiwa kwetu. Utajiri wa mtu hupimwa kwa namna anavyoweza kuwajali wazazi wake kwa kuwahudumia na kuwawezesha kuishi maisha mazuri. Ni kweli kwamba wapo wazazi ambao wamewakosea watoto wao kwa namna moja au nyingine hadi kufikia hatua ya mzazi kumkataa mtoto wake hivyo kusababisha mafarakano, jambo hilo lisikukatishe tamaa na kukuvunja moyo katika kutambua mchango mkubwa alionao mzazi wako katika maisha yako. Mwenyezi Mungu ndiye mgawaji wa Baraka hivyo ataangalia utimilifu wa wajibu wako kwa wazazi wako.
Baadhi yetu wazazi wao wamekwisha tangulia mbele ya haki na kuacha majonzi makubwa katika maisha yao kwani wameondoka kipindi ambacho wanawapenda, wana wajali na kuwahudumia. Fadhila na baraka za mwenyezi Mungu Zitaendelea kuwafuata siku zote za maisha yao na kuwapatia Utajiri ulio mkuu hapa duniani. Hii inatupa fundisho kuwa wakati bado tungali na wazazi wetu tuwatunze na kuwahudumia kwasababu itafika wakati ambao hatutaweza kufanya hivyo. Upo msemo usemao MAJUTO NI MJUKUU hivyo si vizuri tukangoja hatua ambayo tutatamani kuwatendea mema wazazi wetu lakini hatutaweza kutokana na wao kutangulia mbele ya haki.
Mwisho, kipimo kikubwa cha utajiri ni maisha mazuri ya wazazi wetu. Hivyo hatuna budi kuwatengenezea maisha mazuri ambayo watakaa na kufurahia uzao wao hapa duniani. Mzazi atabaki kuwa mzazi hata kama ana mapungufu. Tutumie sehemu ya muda wetu kuwaonyesha upendo na kuwajali na kuwafanya watabamu. Tunapofanya sehemu yetu katika kuwatunza wazazi tunapata baraka na mafanikio katika maisha yetu.
REJEA.
1. QUR'AN TUKUFU SURAT ALBAQARAH
2. BIBLIA TAKATIFU KITABU CHA WAEFESO
3. BONHEIN J.(2018). Kifo na kufa, kuwatunza wazazi wetu wazee.
4. KAMUSI YA KISWAHILI
Wenu
Mwita Ngutunyi mohono
S.l.p 237- Mbarali -mbeya
mwitangutunyimohono@gmail.com

Upvote
37