Kipimo rahisi cha nyota yako

Kipimo rahisi cha nyota yako

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kila mwanadamu ana nyota , ndani yake kuna talanta, na hiyo talanta ndiyo Mungu hutaka mtu aitumie ili asiwe maskini na mhitaji.

Lakini kama ilivyo ada duniani kuna wachawi ambao huchafua nyota za watu au kuibiwa.
Ukiibiwa nyota utateseka mpaka kifo chako.

Hakuna litakalostawi mikononi mwako.

Kama nyota yako iko active, kali , haijaibiwa au kuchafuliwa itest hivi.

Nenda kwenye biashara ya mtu kafanye manunuzi au kapige stori. Ukiona baada tu ya uwepo wako watu wengi wanakuja ujue una nuru /nyota inayong'ara . Watu hufuata nuru. Hata gizani taa ikiwashwa haraka wadudu hujaa.

Ukiona umekaa dk 5 kwenye biashara ya mtu hakuna mtu anekuja mwamba una nyota ndogo sana au umeibiwa tayari
 
Je kama huyo mwenye biashara/ duka nyota yake ikiwq imeshaibiwa au kuchafuliwa!?
Au je kama huyo mwenye duka/biashara nyota yake haijaibiwa Wala kuchafuliwa kwamba ukienda wewe na nyota yako chafu atakosa wateja!!? Wakati umeshasema watu wanafata Nuru
 
Je kama huyo mwenye biashara/ duka nyota yake ikiwq imeshaibiwa au kuchafuliwa!?
Au je kama huyo mwenye duka/biashara nyota yake haijaibiwa Wala kuchafuliwa kwamba ukienda wewe na nyota yako chafu atakosa wateja!!? Wakati umeshasema watu wanafata Nuru
Swali zuri
 
Huyo aliyeenda kwa biashara ya mtu na watu hawakuja ndo mimi...

Alafu mimi huyo huyo nina biashara yangu plas katika biashara yangu akaja mtu hana nyota...

Hiyo inaotwaje kitaalam
 
mimi nikikaa kwenye biashara ya mtu hadi nzi wanaondoka itakuwa nina nyota ya rungu🐼
 
Nimekumbuka zamani wazazi walikuwa wamwambia mtoto wanaedhani ana nyota/kismati awatemee mate mikononi wanapoondoka kwenye utafutaji asubuhi
 
Mwanaume ukiwa na nyota ya chips mayai aisee utawala sana hawa akina dada wasiojitambua
 
Back
Top Bottom