Kipimo sahihi cha CHADEMA sio CCM

Kipimo sahihi cha CHADEMA sio CCM

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Watu wanaoilinganisha CHADEMA na CCM wanakosea na wana uelewa duni wa siasa . Kimuundo au kiutendaji huwezi kuipima CHADEMA dhidi ya CCM, haifai kulinganisha hivi vyama kwa mambo hayo. Utofauti wa hivi vyama huko hivi

CCM ni sawa na serikali au dola, ni vigumu kuchora mstari wa kutenganisha kati ya CCM na serikali. Watu wa CCM wanaingizwa serikalini muda wowote na watu serikali/dola huwa wanaingizwa CCM muda wowote. Hilo haliwezekani kwa CHADEMA.

CCM wanaipa muongozo serikali/dola mambo ya kufanya(ambayo mengine yana maslahi kwa CCM) lakini CHADEMA haina huo uwezo.

CCM ina uwezo wa kutumia dola kuwaajibisha wanachama wake wakati CHADEMA haiwezi kufanya hivyo.

CCM ilithiri mali za serikali na kuzifanya za chama wakati CHADEMA haijawahi kurithi mali za serikali.

CCM ni wasimamizi wa chaguzi huku vyama vingine vyote wakiwa ni washiriki tu wa chaguzi.

Kwa mambo haya na mengine mengi ubora wa CHADEMA kimuundo na utendaji unapaswa kupimwa dhidi ya vyama vingine vya upinzani ila sio CCM chama dola. Labda sera na itikadi tu ndio vitu sahihi kulinganishwa katika hivi vyama, vinginevyo utakuwa unalinganisha maembe na mananasi.
 
Back
Top Bottom