Kipindi bora cha michezo saa 2 asubuhi radio free africa ndio habari ya mjini kwa sasa

Chifyono

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2017
Posts
921
Reaction score
1,659
habari wakuu
nimekuwa mwanamichezo kwa muda sasa huku nikipenda kufuatilia vipindi vya michezo kutoka vyombo vya habari hapa nchini, kwa hakika mwanzo nilivutiwa sana na sport extra ya clouds fm lakini walikwishapoteza dira zaidi wakapigwa gap na e fm (ni kwikwi, hatupoi) ya maurid kitenge

mbali na hivyo vipindi bora kabisa hapa nchini, kipo kipindi bora kabisa kwa sasa hapa nchini kinauchambuzi huru wa kina kimichezo unaoongozwa na Ahmed Ally na wenzake wa redio free africa inayorushwa kutokea ofisi zao ndogo zilizopo kinondoni Dar es salaam.

kimichezo, radio free wamejipanga kurudisha hadhi yao walojijengea hapo awali kupitia kipindi hikio cha michezo kuanzia ya ndani mpaka kimataifa, hongera kwao.

napenda kutoa rai, kipindi hiki kwa sasa hakina wasikilizaji wengi kwa sababu muda(saa 2 asubuhi) kinaoruka hewani wengi wetu tunakua kazini hivyo itapendeza kipindi hiki kirushe majira ya jioni na siku zote katika wiki.

nawasilisha
 
Kwa kweli jamaa wanajitahidi sana. Radio Free Africa,tafadhalini tufikishieni salamu zetu za pongezi kwa Ahmed Ally na wenzake kwa uchambuzi wa kina wa michezo. Eneo la kufanyia kazi hasa kwa Gwamaka na Maregesi ni ngeli, grammar inauma mara kwa mara. Wajitahidi kutumia Kiswahili tu inatosha, huku wakikuza uwezo wao wa lugha ya Kigeni
 
Tatizo la hiyo radio imekuwa ya kuunga unga sana inaweza kuwepo wiki hii hewani ikapotea wiki tatu na kukata kata......siku hizi siipend kwa sababu hiyo ila ikiwaga hewani huwa napenda kusikiliza kipindi cha DJ John cha Solid flash back na kilevcha Alhamis cha Wambura mtani cha Salam za Millenia,RFA ilikuwaga zamani bana
 
Acha utani mkuu, sport extra huwez fananinsha Na vitu vya....
RFA Hata kwa sport headquarters haitii maguu kwanza Ahmed Alii yuko peke ake means akikosekana kipindi hakinogi

Lakini Njoo sport extra wapo full, Hata asipokuwepo huezi ona pengo, tukiacha kwa umoja Wao tumchukue mojamoja,

Hivi kwa mfano unaeza mfananisha Shafii Dauda na nani? Au maestro, au lwambano?
Hiyo miamba utaifanisha na Nani.
Sport extra, Kwangu ni the best sijawai ona
 
Sio kwa kuhamahama huko, ulianza Clouds ukaenda Efm, na sasa RFA na kesho utakua Abood fm kabla ya kwenda Wasaf fm ambapo mwez mmoja mbele utakua Sibuka, na mwez wa kumi uwe standard radio, kabla ya mwaka kuisha utarud Magic na sijui 2019 utaanzia wap!!!!
Yote yote usisahau na ile RTD sasa ni TBC fm
 
Acha utani mkuu, sport extra huwez fananinsha Na vitu vya....
RFA Hata kwa sport headquarters haitii maguu kwanza Ahmed Alii yuko peke ake means akikosekana kipindi hakinogi

Lakini Njoo sport extra wapo full, Hata asipokuwepo huezi ona pengo, tukiacha kwa umoja Wao tumchukue mojamoja,

Hivi kwa mfano unaeza mfananisha Shafii Dauda na nani? Au maestro, au lwambano?
Hiyo miamba utaifanisha na Nani.
Sport extra, Kwangu ni the best sijawai ona
Umesema kweli kabisa,RFA ni redio ya kishamba sana
 
Tatizo la hiyo radio imekuwa ya kuunga unga sana inaweza kuwepo wiki hii hewani ikapotea wiki tatu na kukata kata......siku hizi siipend kwa sababu hiyo ila ikiwaga hewani huwa napenda kusikiliza kipindi cha DJ John cha Solid flash back na kilevcha Alhamis cha Wambura mtani cha Salam za Millenia,RFA ilikuwaga zamani bana
Labda huko kwenu ndio inakatakata wiki tatu
 
Mi kile cha east Africa redio saa mbili usiku kinanikosha sana

Na zamani redio one akiwepo homie kitenge
 
Acha utani mkuu, sport extra huwez fananinsha Na vitu vya....
RFA Hata kwa sport headquarters haitii maguu kwanza Ahmed Alii yuko peke ake means akikosekana kipindi hakinogi

Lakini Njoo sport extra wapo full, Hata asipokuwepo huezi ona pengo, tukiacha kwa umoja Wao tumchukue mojamoja,

Hivi kwa mfano unaeza mfananisha Shafii Dauda na nani? Au maestro, au lwambano?
Hiyo miamba utaifanisha na Nani.
Sport extra, Kwangu ni the best sijawai ona
Ukiona mtu anaponda sports extra ujue huyo ana tatizo Fulani,sababu sijui kama kuna radio yoyote wanayo chambua michezo vizuri zaidi ya clouds.huo ndiyo ukweli halisi
 
Acha utani mkuu, sport extra huwez fananinsha Na vitu vya....
RFA Hata kwa sport headquarters haitii maguu kwanza Ahmed Alii yuko peke ake means akikosekana kipindi hakinogi

Lakini Njoo sport extra wapo full, Hata asipokuwepo huezi ona pengo, tukiacha kwa umoja Wao tumchukue mojamoja,

Hivi kwa mfano unaeza mfananisha Shafii Dauda na nani? Au maestro, au lwambano?
Hiyo miamba utaifanisha na Nani.
Sport extra, Kwangu ni the best sijawai ona
Kwanza Maestro hayupo clouds, yuko EFM kitambo. Pili Shaffih dauda ni mkali wa takwimu na sio uchambuzi na presentation yake sio nzuri na wala hawezi kumfikia Jeff Leah, Oscar Oscar, Mkumbo, Maestro mwenyewe .
 
Kwanza Maestro hayupo clouds, yuko EFM kitambo. Pili Shaffih dauda ni mkali wa takwimu na sio uchambuzi na presentation take sio nzuri na wala hawezi kumfikia Jeff Leah, Oscar Oscar, Mkumbo, Maestro mwenyewe .
Bila kumung'unya maneno, kwa sasa kipindi bora cha michezo redioni ni sports HQ cha e-fm.jamaa wanajitahidi sana kuchambua na kwa sasa kina wachambuzi mahili kabisa. Sports extra ni kweli ilikuwa bora lakini kwa sasa wanazidi kuporomoka
 
Back
Top Bottom