Uchaguzi 2020 Kipindi cha Ajenda 2020 StarTv, Alloyce Nyanda anatumika na CCM au anajikombakomba?

Uchaguzi 2020 Kipindi cha Ajenda 2020 StarTv, Alloyce Nyanda anatumika na CCM au anajikombakomba?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Wapendwa kuna hiki kipindi kinaitwa Ajenda 2020 kinachorushwa kila Jumatatu saa tatu na nusu usiku Startv.

Naona mtangazaji wake aitwaye Alloyce Nyanda anatumika na ccm au yeye mwenyewe anajipendekeza CCM.

Nimekuwa nikimfuatilia kwa kiasi kipindi chake hiki. Nilichokigundua ni kwamba amekuwa akiwachomekea hoja mfu wapinzani ktk kipindi chake halafu anatoa muda mrefu kwa mgeni ambaye ni mwanaccm ili apate kuziponda na kuzizodoa hoja hizo huku na yeye akimsapoti mwanaccm.

Kwa maoni yangu, kukosekana kwa weledi huko watangazaji wa kibongo wa enzi hizi wataendele kupakaa poda tu usoni lkn hawatakuwa mahiri duniani.

Wamejaa utoto na kujipendekeza kwa serikali kulikopiitiliza na hivyo kuifanya fani hii ikose heshima yake.

Katika kipindi hiki cha kampeni nashauri wapige marufuku viongozi wao kuhudhuria mijadala yoyote inayoendeshwa na kipindi hiki.
 
Bado mnaangali startv hasa kipindi Kama hiki? Mna moyo aisee.

Media zote zimeshikwa kalio zikiinama nchale' zikikenua 'nchale' usitegemee utakuta story zitakuwa balanced

Mkuu nilidhani labda hawa StarTv hawana ndoa na CCM nikawa nafuatilia vipindi vyao. Lkn kwa kweli wamekamatwa makalio kqma ulivyosema.
 
Nadhani ushasahau issue yao ya kurusha matangazo yao ya moja kwa moja kupitia BBC Swahili.

Hii ya kuita na kuwahoji upinzani Ni Tia maji Tia maji ili wasipoteze watazamaji kiduchu waliobaki.
 
Ila nmeona kipindi cha leo kimekatika bila muda kufikia tamati,mchuano ulikuwa mkali kiasi.
Kuhusu hoja yako sina uhakika nayo ila nlichoona jamaa kuna mahala kwenye namna ya uulizaji maswali ndo nmeona changamoto.
 
Mimi nilidhani uta hoji kipindi cha leo kukatika hewani bila sababu...
 
Mwandishi Nguli kwangu mimi atabaki kuwa Doto Bulendu hawa wengine makajanja tu​
 
Mkuu niwe fair kwa huyo Aloyce Nyanda, huwa anajitahidi kubalance habari za wapinzani, najua hawezi kabisa maana mazingira sio rafiki, na wote hili tunalijua. Wangalau Star Tv ndio huwa wanawaalika wapinzani. Usiku huu kwenye hicho kipindi kulikuwa na diwani wa ccm mstaafu, na katibu wa Cdm kanda ya ziwa kama sikosei. Mjadala ulikuwa moto, ila katika hali ya kushangaza na niliyoitarajia, kipindi hicho kimekatingiza matangazo yake ghafla!

Hayo ndio mazingira ya vyombo vya habari. Huenda Nyanda au huyo katibu wa Cdm akatoa ufafanuzi wa kilichotokea.

cc: Paskali Mayalla
 
😂 jamaa kaja studio na makaratasi ya lawama kumbe makaratasi ya fidia ya kubomolewa nyumba.

Nilicheka mno
😂😂😂😂😂😂😂
 
Sijawahi kuelewa kabisa.na sitakielewa mpaka siku ya mwisho
 
Mkuu niwe fair kwa huyo Aloyce Nyanda, huwa anajitahidi kubalance habari za wapinzani, najua hawezi kabisa maana mazingira sio rafiki, na wote hili tunalijua. Wangalau Star Tv ndio huwa wanawaalika wapinzani. Usiku huu kwenye hicho kipindi kulikuwa na diwani wa ccm mstaafu, na katibu wa Cdm kanda ya ziwa kama sikosei. Mjadala ulikuwa moto, ila katika hali ya kushangaza na niliyoitarajia, kipindi hicho kimekatingiza matangazo yake ghafla!

Hayo ndio mazingira ya vyombo vya habari. Huenda Nyanda au huyo katibu wa Cdm akatoa ufafanuzi wa kilichotokea.

cc: Paskali Mayalla
Diwani mstaafu kachezea spana balaa 😂😂😂. Halafu jamaa wa chadema katumia fursa akiwa live kwenye Tv kutangaza Lissu anatua Mwanza kesho.
Baada ya hapo matangazo yakakatika.😂😂

Lini Lissu Anakuja Kagera?(wenye ratiba tupeni majibu)
 
Mkuu niwe fair kwa huyo Aloyce Nyanda, huwa anajitahidi kubalance habari za wapinzani, najua hawezi kabisa maana mazingira sio rafiki, na wote hili tunalijua. Wangalau Star Tv ndio huwa wanawaalika wapinzani. Usiku huu kwenye hicho kipindi kulikuwa na diwani wa ccm mstaafu, na katibu wa Cdm kanda ya ziwa kama sikosei. Mjadala ulikuwa moto, ila katika hali ya kushangaza na niliyoitarajia, kipindi hicho kimekatingiza matangazo yake ghafla!

Hayo ndio mazingira ya vyombo vya habari. Huenda Nyanda au huyo katibu wa Cdm akatoa ufafanuzi wa kilichotokea.

cc: Paskali Mayalla

..kuna siku LAlloyce Nyanda alimhoji Mh.Sugu.

..kwa kweli nilimuonea huruma sana.

..nadhani hatarudia tena maishani mwake kumhoji Sugu.

NB:

..kila anapofanya mahojiano na viongozi wa upinzani lazima awalazimishe wamsifie Magufuli.
 
Diwani mstaafu kachezea spana balaa [emoji23][emoji23][emoji23]. Halafu jamaa wa chadema katumia fursa akiwa live kwenye Tv kutangaza Lissu anatua Mwanza kesho.

Lini Lissu Anakuja Kagera?(wenye ratiba tupeni majibu)
Hahahaaa hata mimi ile nimeikubali...

Diwani mstaafu alikuwa anahojiwa na watu wawili...

Yawezekana simu kutoka juu imehusika, ndio maana matangazo yalikatika njiani...
 
Hahahaaa hata mimi ile nimeikubali...

Yawezekana simu kutoka juu imehusika, ndio maana matangazo yalikatika njiani...
😂. Yaani wakati jamaa wanaendelea kutiana spana. Nyanda alikuwa anageukageuka halafu sura yake kama anapokea maelekezo kutoka nyuma ya Camera. Mara ghafla sura ikaanza kuvimba hivi kama mtu anayetaka kulia. Mara ghafla akasema kuna tangazo ndio ikawa mazima hiyo. Ikaja documentary sijui ya nchi gani huko barabara mbovuuuu magari ya mahindra. Kipindi kikayeyuka. 😂😂
 
Hata Mimi nilitegemea kinaendelea halafu mwisho wa siku star TV wametuacha kwenye mataa hoja zilizoibuliwa hapo ilitakiwa zijibiwe vizuri
 
😂 jamaa kaja studio na makaratasi ya lawama kumbe makaratasi ya fidia ya kubomolewa nyumba.

Nilicheka mno
😂😂😂😂😂😂😂
Hili ndiyo limeniboa mm. Maana nikaona mtangazaji anambeba huyo mwenye makaratasi feki azidi kumwaga umbea wake
 
😂. Yaani wakati jamaa wanaendelea kutiana spana. Nyanda alikuwa anageukageuka halafu sura yake kama anapokea maelekezo kutoka nyuma ya Camera. Mara ghafla sura ikaanza kuvimba hivi kama mtu anayetaka kulia. Mara ghafla akasema kuna tangazo ndio ikawa mazima hiyo. Ikaja documentary sijui ya nchi gani huko barabara mbovuuuu magari ya mahindra. Kipindi kikayeyuka. 😂😂
Itakuwa jiwe kasikia yule katibu wa Kanda akitumia fursa kutangaza mkutano wa Lisu Mwanza hapo kesho. Jiwe amefura balaa
 
Hili ndiyo limeniboa mm. Maana nikaona mtangazaji anambeba huyo mwenye makaratasi feki azidi kumwaga umbea wake
Nilidhani karatasi zina bonge moja la ushahidi. Tena mzito balaa. Kumbe ni fidia ya nyumba iliyobomolewa Kakola mwaka 1996 😂😂 aisee ningekuwa mtangazaji ningecheka hapo hapo studio. Halafu jamaa anavyojiamini anasema ametunza ushahidi wa miaka zaidi ya 20 na kasisitiza wasome na ya pili. Kusoma karatasi ya pili na yenyewe ni watu waliobomolewa nyumba zao na mgodi miaka hiyooo. 😂😂

Jamaa aliishiwa nguvu akaegamia kiti yaani akasinyaa ghafla. Kisha jamaa wa cdm akamgeuzia gia angani jinsi jamaa alivyoleta ushahidi wa jinsi walivyonyanyaswa na ccm. 😂😂

Niliona diwani weusi unamkolea zaidi. Yaani wasingekata matangazo ilikuwa ni vichekesho bora wamemuokoa diwani. 😂
 
Back
Top Bottom