Kipindi cha Bunge kina matangazo mengi yanayopoteza muda

Kipindi cha Bunge kina matangazo mengi yanayopoteza muda

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Bungeni kumekuwa na matangazo mengi na inasababisha muda wa maswali na majibu au kujibu hoja kuwa mdogo. Unaweza ukadhani ni kipindi cha michezo iliyojaa matangazo kila baada ya dk 3.

Mfano utambulisho wa wageni usio na tija, wageni kama timu ya mpira kufanya vizuri kupongezwa ni sawa ila utambulisho wa wageni wa wabunge na mawaziri haina tija ni kupoteza muda.

Unakuta wanafunzi wa shule, wageni wa wabunge na wake zao, mawaziri, wenyeviti wa vijiji, wanavyuo, madiwani, taasisi na watu ambao hawahusiki na mjadala wa bungeni.

Haya ni matumizi mabaya ya muda halafu kwenye maswali ya msingi spika anawapeleka fasta wakati muda wa kutosha umepotea kwenye utambulisho.
 
Wewe una roho ngumu sana, mimi siwezi kusikiliza bunge la upotoshaji hata siku 1
 
Muda uliotumia kuandika hii post sio matumizi mabaya ya muda.?
 
Muda uliotumia kuandika hii post sio matumizi mabaya ya muda.?
Nimeandika kwasababu ni kitu kinachojirudia kila siku, bunge siyo sehemu ya kutafuta ujiko na kuuza sura kama huhusiki
 
nimeandika kwasababu ni kitu kinachojirudia kila siku,bunge siyo sehemu ya kutafuta ujiko na kuuza sura kama huhusiki
Hata mimi, huwa nakerwa sana na hii tabia. Wangetenga siku maalum kwa ajili ya wageni, kuliko hivi, kuna athiri ratiba za
Kila siku!
 
Hata mimi, huwa nakerwa sana na hii tabia. Wangetenga siku maalum kwa ajili ya wageni, kuliko hivi, kuna athiri ratiba za
Kila siku!
Yeah mkuu !

Katikati ya mjadala unashangaa spika anaanza kutambua uwepo,unaona anavyobana mda kumbe anawahi kwenye utambulisho
 
Back
Top Bottom