Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,053
- 6,304
Baada ya ukimya kutawala kwenye TV station kwa juma la pili maswali mengi yameulizwa na wadau wa kipindi cha In My Shoes ambacho kilikuwa kinaonyesha uhalisia wa Maisha ya Wema Sepetu na kurushwa na kituo cha EATV.
Ukimya huo ulizua taswira kwa fans wa Wema Sepetu na kutaka kujua kulikoni kipindi kutokuwepo hewani kuwa amefulia au la? Bk iliamua kuzungumza na Maneger wa Wema, Martin Kadinda ili kuelezea juu ya sababu zinazofanya kipindi hicho kuto uonekana.
Haaaaaa wapi wewe nani kasema, Wema hajafulia wewe unaona kuna mtu wa kufulia pale? ni kwamba mkataba ambao Wema alikuwa amesaini na EATV umeisha mpaka baada ya miezi mitatu ndipo kipindi kitarudi tena hewani.
BK: liliendelea kumtwanga maswali Martin kuwa labda kwa sasa Wema anazichangachanga kwanza then arudi tena baada ya mshiko kuwa poa?
Hapana Wema wakati anasaini mkataba alikuwa anajua kuwa kuna kipindi ambacho kinatakiwa kuanza mwezi wa nne ambacho ndicho hicho kilichochukua nafasi ya In My Shoes lakini kipindi cha The Baloziz kinatarajiwa kuisha baada ya miezi mitatu ndipo Wema atakapo rudi tena. Martin