Kipindi cha Ngazi Kwa Ngazi by Salama Jabir

MH! labda location ndio bomba but kipindi mi binafsi sijaona jipya labda kama ameamua kutujulisha miziki yake pendwa, angetuambia tu ni salama best hits, maana mbwembwe tu, labda ule upaja uliokaa wazi ndani ya kaptura utakuwa unavuta watizamaji akiifanya ile kaptula ndio uniform ya kipindi.
 
Kibovu hakina jipya..hizo nyimbo na komedi alizoweka tushaziona kitaaamboo..binafsi sijaelewa hata lengo la kipindi..wakiboreshe salama.si wa kuendesha kipindi kilichopooza kama kile
Kwann unasema salama hafai kuendesha hicho kipindi
 
Kipindi ni kizuri na kipo tofauti sana na kimebeba vitu vingi ndani ya saa moja kupata ladha tofauti.

Arabian music (eg. Amr diab)
Indian music (eg. Shah rukh khan)
Nigeria, Kenya, American music, Bongo fleva na dunia nzima kwa ujumla. Part ya mtazamaji kuchagua kichekesho na kuonekana live.

Ametoa shout out kwa video za bongofleva na wasanii wa bongo sio kama zamani wakati yupo planet bongo. Pia nimeona anaepuka mambo udaku, team, gossip, umbea na ubuyu kushow lov na kuweka utofauti na vipindi vingine vilivyozoeleka East Africa

Salama ni mtangazaji mzoefu anajua sana yupo free na anatiririka kutema madini kutoka duniani kote. Location pia nzuri sana
Big up Salama, keep it up!!
 
Wafanye utaratibu Eatv iwepo kwenye dstv..nacc tufaidi
Ila nadhani kipindi kibaya au ndio vle kama bigG vinakuja mwanzo vzr mwisho vinapotea
 
Hichi kipind kwako umekuonaje..?
kipo kawaida kajalibu kuonesha utofauti lakin bahati mbaya amefeli ata sammisago kampiga gap anachukua clip zakila siku yeye salama mpaka arecord vipind kadhaa me nadhan mkasi angewarudia walewale wasanii kipind kimepwaya sana ata kwenda youtube ni ngumu clip zile zile video zile zile
 
Kwakweli binafsi sijakielewa, hizo top 20 nyingine za mwaka 47 nyingine za juzi yaani ilimradi tu, ni bora angeita chaguo la dj ningeelewa maana anaweka nyimbo anayojisikia, halafu kachanganya mavitu kibao hadi unasahau kipindi kinahusu nini. Na kawaida ya kukubali kila Salama anachofanya ila hapa ubunifu wake sijaukubali, naunga mkono wenzangu waliosema kwamba location na graphics zimetulia, nimependa kale ka animation ntamtafuta aliyekatengeneza anifundishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…