Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
daaah, yaani I ulichopost hapa unge type kwenye google mbona saa nyingi ungekuwa unatupa ma info ya kufa mtu hapa
Habari zenu wana JF, naomba kuuliza hivii.. mtangazaji wa Clouds FM Dr. Issack Maro anayeendesha kipindi cha njia panda, ametozwa faini kiasi gani na hivi analipa yeye mwenyewe au inalipwa na ofisi.
Ni hayo tu waungwana.
Unatuuliza sisi unadhan tutakua na majibu sahihi??? Daah jf ina vimbwanga vyake.
Nenda pale mikocheni ofisini kwao ndo wanaweza kukupa jibu sahh
Katozwa faini kwa kosa gani ?
Katozwa faini na nani? Kwa kosa gani? Ilikua lini? Maro Ni nani na dr wa nini?
pole sana chifu77
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005.
Wakielezea uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Margaret Munyagi ilisema kuwa ukiukwaji wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati tofauti na vituo hivyo.
Alisema kwa upande wa kituo cha redio cha Clouds, kupitia kipindi chake cha Njia Panda kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka huu kati ya saa 8.00 mchana na saa 10.00 jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya kuzimu ambapo maudhui yake yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na kichawi.
Aidha alisema kosa lingine kituo hicho hakikufuata kanuni za Utangazaji(maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya vipindi vyao kwa TCRA ili viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo kipindi cha Njia Panda hakikuwasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa.
Wakati huo huo, kituo cha televisheni cha Clouds kilirusha kipindi cha Bibi Bomba Mei 16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na saa 4.00 usiku ambacho kilikiuka kanuni za Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005.
Alisema kipindi hicho kilidhalilisha mabibi hao walioshiriki pamoja na wanawake kwa ujumla kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni hizo.
Aidha alisema kituo hicho kinatozwa faini ya Sh milioni moja na kutakiwa kuwasilisha TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa kabla ya kutangazwa.
TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mmmm sasa huyu jamaa hamnazo kabisa... @ mawenzi
kwa taaluma yake huwa anajua kabisa waganga wanadanganya ila anaendelea tu sababu ya pesa.Nashukuru sana kwa TCRA kuyaona makosa hayo ya Clouds. Kosa lingine la Clouds ni kuwa partisan as far as politics za TZ is concerned. The stations are openly pro CCM. Je hii inaruhusiwa kwa chombo cha habari?
Kuhusu Dr Isaac Maro, ni kwamba anaidhalilisha hata taaluma yake ya u-Medical Dr. Utakuta anawaita waganga wa kienyeji na kuwafanyia interview ndefu huku akiwaita "Dr". Je huku si kuwafanyia promo at no cost? Au cost anapewa yeye binafsi? Anakitumia vibaya sana kipindi cha Njia Panda, kwa manufaa yake binafsi. Tofauti kabisa na mwanzilishi wa kipindi hiki ambaye naye alikuwa Medical Doctor. Uongozi wa Clouds unabidi uwe macho saana na huyu kijana. Mengi anayofanya ni kwa maslahi binafsi.
Wakati serkali inafikiria kupiga marufuku matangazo ya waganga wa kienyeji, yeye ndiyo kwanza anaitumia Clouds kuwapa promo, hasa wale wanaodai kutibu vidonda vya tumbo. Anahongwa na hao waganga feki.