Kipindi cha njia panda na Issack Maro

chifu77

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2014
Posts
902
Reaction score
596
Habari zenu wana JF, naomba kuuliza hivii.. mtangazaji wa Clouds FM Dr. Issack Maro anayeendesha kipindi cha njia panda, ametozwa faini kiasi gani na hivi analipa yeye mwenyewe au inalipwa na ofisi.

Ni hayo tu waungwana.
 
daaah, yaani I ulichopost hapa unge type kwenye google mbona saa nyingi ungekuwa unatupa ma info ya kufa mtu hapa
 
Yaani hata huwa sifuatilii hicho kipindi

Mkuu tujuze basi Kafanyaje manaake sio wote tunajua humu
 
Mkuu client3 tujuze basi... funguka mzazi tunakusubiria.
 
daaah, yaani I ulichopost hapa unge type kwenye google mbona saa nyingi ungekuwa unatupa ma info ya kufa mtu hapa

Mkuu nimetype kwenye google wala sijaona chochote huko.. naomba hiyo linki unayosemea wewe ili nijaribu tena..
 
Unatuuliza sisi unadhan tutakua na majibu sahihi??? Daah jf ina vimbwanga vyake.

Nenda pale mikocheni ofisini kwao ndo wanaweza kukupa jibu sahh
 
Habari zenu wana JF, naomba kuuliza hivii.. mtangazaji wa Clouds FM Dr. Issack Maro anayeendesha kipindi cha njia panda, ametozwa faini kiasi gani na hivi analipa yeye mwenyewe au inalipwa na ofisi.

Ni hayo tu waungwana.

Katozwa faini na nani? Kwa kosa gani? Ilikua lini? Maro Ni nani na dr wa nini?
 
Unatuuliza sisi unadhan tutakua na majibu sahihi??? Daah jf ina vimbwanga vyake.

Nenda pale mikocheni ofisini kwao ndo wanaweza kukupa jibu sahh

Mkuu kwangu mimi kuuliza hapa JF ndo rahisi kwangu. Ni ngumu kwenda huko dar, mie naishi dodoma. Teknologia ya mawasiliano inawezesha kufanya haya hamna haja ya kwenda dar.
 
Kalagabaho.. maswali yako ni mengi.. vuta subira ngoja wanaofahamu waje kutusaidia....
 
Unajua tena njia panda lazima usimame,uangalie kulia alafu kushoto,jamaa alipita kwa kasi sana trafiki wakamuona speed 80 ilikuwa hatari sana,wamempiga faini elfu 30.
 
pole sana chifu77

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005.

Wakielezea uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Margaret Munyagi ilisema kuwa ukiukwaji wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati tofauti na vituo hivyo.

Alisema kwa upande wa kituo cha redio cha Clouds, kupitia kipindi chake cha ‘Njia Panda' kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka huu kati ya saa 8.00 mchana na saa 10.00 jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya kuzimu ambapo maudhui yake yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na kichawi.

Aidha alisema kosa lingine kituo hicho hakikufuata kanuni za Utangazaji(maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya vipindi vyao kwa TCRA ili viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo kipindi cha Njia Panda hakikuwasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa.

Wakati huo huo, kituo cha televisheni cha Clouds kilirusha kipindi cha ‘Bibi Bomba' Mei 16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na saa 4.00 usiku ambacho kilikiuka kanuni za Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005.

Alisema kipindi hicho kilidhalilisha mabibi hao walioshiriki pamoja na wanawake kwa ujumla kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni hizo.

Aidha alisema kituo hicho kinatozwa faini ya Sh milioni moja na kutakiwa kuwasilisha TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa kabla ya kutangazwa.

TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru sana kwa TCRA kuyaona makosa hayo ya Clouds. Kosa lingine la Clouds ni kuwa partisan as far as politics za TZ is concerned. The stations are openly pro CCM. Je hii inaruhusiwa kwa chombo cha habari?

Kuhusu Dr Isaac Maro, ni kwamba anaidhalilisha hata taaluma yake ya u-Medical Dr. Utakuta anawaita waganga wa kienyeji na kuwafanyia interview ndefu huku akiwaita "Dr". Je huku si kuwafanyia promo at no cost? Au cost anapewa yeye binafsi? Anakitumia vibaya sana kipindi cha Njia Panda, kwa manufaa yake binafsi. Tofauti kabisa na mwanzilishi wa kipindi hiki ambaye naye alikuwa Medical Doctor. Uongozi wa Clouds unabidi uwe macho saana na huyu kijana. Mengi anayofanya ni kwa maslahi binafsi.

Wakati serkali inafikiria kupiga marufuku matangazo ya waganga wa kienyeji, yeye ndiyo kwanza anaitumia Clouds kuwapa promo, hasa wale wanaodai kutibu vidonda vya tumbo. Anahongwa na hao waganga feki.
 

Kwanza saluti kwako Mkuu client3, pili nashukuru sana.. mie kwa mtazamo wangu nilijia TCRA wameamua kuuvuta upanga kwa sababu tu wao wameshika mpini.
 
Last edited by a moderator:
Mmmm sasa huyu jamaa hamnazo kabisa... @ mawenzi
 
Mmmm sasa huyu jamaa hamnazo kabisa... @ mawenzi

Isaac Maro ni tapeli fulani anayetumia taaluma ya u-MD kwa kutumia Clouds kujinufaisha binafsi. Vipindi vyake vingi vina harufu ya utapeli ambao utawala wa Clouds siyo rahisi kuugundua. chifu77
 
Last edited by a moderator:
kwa taaluma yake huwa anajua kabisa waganga wanadanganya ila anaendelea tu sababu ya pesa.
 
Matatizo hayo ya kinakusaga kuajiri vilaza.Juzi kati nekwenda hapo clouds mikocheni.....nikafika na kumkuta receptionist wa kiume ambaye hajui maadili ya kazi yake.Eti namwambia nataka kuonana na meneja wa vipindi vya television nahitaji kupata maelezo yake binafsi jinsi ya kufanya kipindi jipya hapo clouds tv......jamaa akaniambia niketi nisubiri kidogo....zimepitaka kama dk20 hivi nikamuuliza vipi jamaa yupo tyt sana nini nije siku nyingine.....akanijibu eti nimemtext bado hajajibu........nilipatwa na hasira nikasepa bila kuaga nikasema hii idea yangu bora nipeleke tbc kulikoni hawa maboya wenye dharau kiasi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…